Showing posts with label FREEMASON. Show all posts
Showing posts with label FREEMASON. Show all posts

January 18, 2014

HIKI NI KIZAZI CHA NYOKA KILICHOLAANIWA MSANII KANYE WEST AANZISHA DINI YAKE IITWAYO YEEZIANITY YEYE AJIITA NI MUNGU WA DINI HIYO

Hi | 7:22:00 PM | | | Be first to comment
 Kanye West amepata dini yake iitwayo Yeezianity, “I AM a God,” Kanye West anasikika kwenye moja ya nyimbo zake zilizopo kwenye album Yeezus (jina likiwa mchanganyiko wa aka ‘Ye – na Jesus).
Na sasa wafuasi wa rapper huyo wameanzisha website, Yeezianity.com maalum kwa watu wote wanaotaka kubadilisha dini kwenda Yeezianity, inayojitangaza kama “THE BEST CHURCH OF ALL TIME!
“Sisi ni kundi lisilotaka kujulikana linaloamini kuwa yule anayejiita Yeezus ni kiumbe kitakatifu kilichotumwa na Mungu kuongoza kwenye kizazi kipya cha ubinadamu,” yanasomeka maneno kwenye website.

Kwenye website hiyo kuna sheria kadhaa au nguzo na tamko la imani likiwemo ‘Imani kwa Yeezus’ na ‘I believe Yeezus will lead us into a new Age of Creativity’. Amen.” Mwanzilishi wa ‘Yeezianity’ ameongea na mtandao wa Vice kwa masharti ya kutotajwa jina na kusema kuwa Yeezianity si kitu cha mzaha
 Ukitaka kujiunga na dini hiini rahisi sana.Unachotakiwa kufanya ni kuwatumia email yenye picha isiyokutambulisha ukiwa umeshika karatasi lililoandikwa ‘I Believe In Yeezus’.

October 23, 2013

BREAKING NEWS..! ASKOFU MPENDA ANASA MJERUMANI TEBARTZ VAN ELST ASIMAMISHWA VATICAN

Hi | 2:56:00 PM | | | Be first to comment
Mchana huu, Vatican imemsimamisha kazi askofu mpenda anasa Mjerumani, Tebartz-van Elst, aliyetumia TSh 68 bil za kanisa kujenga jumba la fahari..
Endelea kuperuzi mtandao wetu kwa habari zaidi.

April 13, 2013

SIR ANDY CHANDE ASEMA TANZANIA INA WANACHAMA HAI ZAIDI YA 600 WA KUNDI LA WATU WENYE IMANI YA SIRI FREEMASONS

Hi | 9:02:00 PM | | Be first to comment

Sir Andy Chande Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600 wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na watu wa kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku ikielezwa kwamba miongoni mwao hakuna viongozi wakuu wa serikali..

Hayo yalibainishwa na Kiongozi wa kundi la Freemasons katika eneo la Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande alipozungumza na gazeti hili, wiki hii Dar es Salaam. Kiongozi huyo Mtanzania mkazi wa Dar es Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema licha ya Tanzania kuwa na wanachama hao, kwa sasa idadi ya wanachama duniani inapungua tofauti na inavyoonekana sasa kuwa wanaongezeka kutokana na kuibuka maneno mengi kuhusu kundi hilo. 

December 8, 2012

SASA MAMBO WAZIWAZI WAPENDA PESA HII NI KWA WASIOPENDA KUJITUMA FREEMASON WATINGA BILA KUJIFICHA ENEO LA KILIMAHEWA WILAYANI ILEMELA JIJINI MWANZA

Hi | 4:25:00 PM | | Be first to comment
Ni bango lililotundikwa eneo la Kilimahewa wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Kuhusu mawasiliano ambayo yameandikwa chini mwishoni mwa karatasi hiyo ni
0655 905 559
0756 520 154
0789 905 559
0222 405 682
 

Chunguza kwanza ili isije ikakugharimu mdau usidanganyike na tamaa ya vishawishi vya pesa!! Hakuna faida yeyote utakayokuwa nayo kwa kutumia pesa za kimiujiza ambazo hujazitolea jasho. Mwisho

October 9, 2012

TASWIRA ZA MAZISHI CHA GEORGE ALIYETOA USHUHUDA WA KANUMBA KUWA AMEUAWAWA NA FREEMASON

Hi | 5:35:00 PM | | | Be first to comment
 Mwili wa George Kairuki.

Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'
TAARIFA zilizotufikia wakati  tunakwenda mtamboni zinadai kuwa, yule kijana aliyefahamika kwa jina la George Nimayou ambaye siku za nyuma aliibuka na kudai marehemu Steven Kanumba alikuwa freemason, amefariki dunia ghafla.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilichoomba hifadhi ya jina, kijana huyo alifariki dunia Septemba 29, mwaka huu huko Tabata jijini Dar alikokuwa akiishi na kifo chake kinafananishwa na kile cha marehemu Kanumba.
Chanzo hicho kilidai kuwa, siku ya tukio zilisikika kelele ndani ya chumba alichokuwa akiishi na baada ya muda alitoka mwanamke na kutokomea kusikojulikana.

“Hatukujua kilichotokea, tulipoingia ndani tukakuta George amekufa ndipo taratibu za mazishi zilipofanyika,” kilidai chanzo hicho.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya watu wanaoishi eneo hilo walieleza kushangazwa na tukio hilo huku baadhi wakishindwa kuamini na kuhisi huenda alikuwa anarekodi filamu.

“Na sisi tunasikia tu kuwa eti kafariki lakini mbona msiba wenyewe hatukuusikia na hata picha za tukio zinaonesha watu wachache sana, sisi tunahisi kuna kitu nyuma ya tukio hili, hatuamini kuwa amekufa, “ alisema Mariam Hassan wa Tabata.

Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa maofisa wa polisi Mkoa wa Ilala ambaye hakupenda jina liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo ambapo alisema, hawajapata taarifa ya tukio hilo na kwamba huenda ni uzushi hivyo waandishi wetu wanaendelea kuifuatilia kwa kina, ikikamilika itaenda hewani.

July 29, 2012

SECRET HISTORY OF THE FREEMASONS(HISTORIA YA SIRI YA FREEMASONS):DOCUMENTARY

Hi | 12:52:00 AM | | Be first to comment
This documentary provides insights into Freemasonry. Although Freemasonry claims to not be a religion, documentary evidence proves otherwise. In fact, Masonic literature and doctrine exposes Freemasonry as a Luciferian religion. Lucifer is the 'god' of Freemasonry. (Albert Pike, Morals & Dogma). Albert Pike also reveals that the initiates of Freemasonry at the lower degrees are in fact deceived.

Furthermore, Masonic doctrine is based on esoteric occult knowledge that is designed to 'enlighten' it's initiates. Essentially, the aim of a Mason is to become 'born again' through secret knowledge. This is achieved by becoming a better person through the knowledge imparted to the initiates of Freemasonry as they rise through the degrees or levels of initiation and doctrinal teachings.

Masonic teachings are nothing less than an elaborate counterfeit of the Bible. It is a religion of secularism and has its roots in ancient Babylonian false religion found in the Old Testament of the Bible. It propagates the lie of Satan in the Garden of Eden that man can in fact become a 'god' and that this status is attained by eating of the Tree of Knowledge. By contrast, Yahweh (God) teaches in the Bible that the only way that fallen man can be born again (spiritually), is through the redemptive work and person of Jesus Christ. Man does not have the power to 'save himself' and needs a redeemer who has the power over sin and death.

One of the aims of Freemasonry is to rebuild the Temple of Solomon in Jerusalem. Lucifer (Satan) has established his counterfeit secular humanistic pagan religion (Freemasonry), to 'build' his kingdom on the earth. The Bible teaches that Satan is in fact the Prince of this world but that his power and control over the earth and the people of the earth is temporary. Satan's plan is ultimately to seat himself in the rebuilt Temple of Solomon in Jerusalem. The false prophet who will be revealed at the end of the age, and just before the return of Jesus Christ, will enthrone himself as God in Jerusalem. For a period of time, the nations of the world will worship him as God.

This is the ultimate deception and insult to the living God (Yahweh). It is also what is described as the Abomination of Desolation in the Book of Daniel in the Bible.
Jesus Christ will eventually return to the earth to establish his eternal rule over the nations, principalities and powers of the earth. The Kingdom of God will be established on the earth and Christ will govern his Kingdom from the New Jerusalem that comes down to earth from Heaven.
INSIDE FREEMASONRY(DOCUMENTARY)
An unique and intimate interview with a few Freemasons who discuss the Lodge from the inside. As well as viewpoints from Prince Hall Freemasons
Ni wazi kwamba BC haishabikii wala haifungamani kwa njia yeyote ile na imani ya Freemasons(misimamo yetu inaeleweka bila shaka). Pamoja na hayo, BC ni chombo au daraja la kuelimishana.Isitoshe, kwa muda sasa kumekuwa na upotoshaji mwingi,mara nyingi,kupitia vyombo mbalimbali vya habari(hususani magazeti) kuhusiana na suala zima la imani ijulikanayo kama Freemasons,tunaamini kwamba sio vibaya endapo BC itatumika kama chombo au daraja la kusaidia kupatikana kwa elimu au maarifa ya aina fulani juu ya jambo husika. Ndio maana hapa chini unaweza kutizama documentary(takribani masaa mawili hivi) kuhusu historia ya siri ya Freemasons.

Najua ingependeza zaidi kama documentary hii ingekuwa na tafsiri ya lugha ya Kiswahili.Kwa bahati mbaya,ipo katika Kiingereza.Hata kama kiingereza sio lugha unayoielewa sana,jaribu tu kuitazama.Kama huwezi kabisa kuelewa,basi mtafute mtu ambaye anaelewa zaidi akusaidie kuelewa.

July 14, 2012

MAJADILIANO KATIKA MITANDAO YA KIJAMII FACEBOOK: TASWIRA ZA UKWELI WOWOTE KUHUSU KANUMBA NA FREEMASON?

Hi | 11:23:00 AM | | Be first to comment
Hii Picha Ndiyo Iliyotumika Kwenye Msiba ndo Ilikuwa Mbele Ili Mtu Kuweza Kumtambua Marehemu. Ukitazama Shati hapo Katikati kuna alama ya fuvu na namba 13, na kwenye fuvu sehemu ya Ubongo Kuna Tobo Kuonesha Ishara wadadisi wa mambo wanasema ni Kuonesha "Brain Itatikisika" na kwenye Mdomo Kuna tobo Kuonesha kuna kitu kitatoka mdomoni....hizi ni Tafsiri za Wataalam.
Hapa alikuwa amepiga Picha na kwenye Kiti Kuna alama ya Mojawapo ya Illuminati Syombols.

Hapa ndipo Mjadala wa Chini Ukaibuka.
Mwenye Picha Nzuri Ya Jeneza la Kanumba Tafadhari naomba ani tag....nataka tazama je ni kweli Kwenye zile picha zilizochorwa kwenye jeneza kama Urembo Kuna alama ya Fuvu na namba 13?na Kama kuna uhusiano wowote wa ki-masonic kufa tarehe 7, Saa 7 na jina lake lenye Nyota Kanumba kuwa na Herufi 7??then nitazame uhusiano wa Movie ya Devil's Kingdom.

July 7, 2012

TUJIKUMBUSHE NA YULE MTANZANIA ALIYETANGAZA KUJITOA KATIKA DINI YA FREEMASONS ALIYEPIGWA MHURI WA CHUMA MGUUNI.

Hi | 6:46:00 PM | | Be first to comment
Japokua anadai alikua mwanachama wa FREEMASONS, Samwel alikua anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya pia na amekiri kufanya biashara hiyo na baadhi ya viongozi wakubwa wa dini wa Tanzania na hata kukaa nao meza moja, hiyo alama kwenye sikio lake la kulia anasema waliwekewa kwa makusudi ili iwe rahisi kutambulika popote atakapotokea, yani ukimuona tu unajua huyu anauza hizo dawa za kulevya.
Hii ndio anasema ni alama kubwa aliyopigwa katika mguu wake wa kushoto kumtambulisha kwamba ni mwanachama wa FREEMASON, ni alama kama muhuri, iliyoambatana na KIAPO ambapo popote atakapokwenda atatambulika, amesema kwa sasa ndio inamsumbua sana kwa sababu chuma kilichotumika kumuwekea kimevunja mfupa, na hii aliifanya huko Afrika Kusini.
 
Samwel amesema alikimbia na kujiondoa kwenye dini hiyo inayodaiwa kuwa ya kishetani baada ya kutoka gerezani huko Afrika kusini, walikua wanatumwa kwenda kuua wat kwenye ajali na sehemu nyingine, walipewa irizi maalum ambapo baada ya kuona hayawezi hayo maisha akakimbia lakini mpaka sasa hivi anakiri kwamba anatafutwa kwa sababu ndio alikua anamalizia hatua ya mwisho kuingia kwenye hatua ya kutajirishwa kwa mali kama inavyotokea kwa waumini wengine, ila akatoroka na baadae ndio akasikia jamaa aliempeleka kwenye hiyo dini nae ameuwawa baada ya kugundulika kwamba alikua anataka kujiondoa.

Samwel anasema amewahi kwenda kwenye kanisa la FREEMASON hapa Dar es salaam Posta mara moja tu na kukutana na watu kadhaa maarufu wabongo ambao leo jumatatu ya march 19 2012  kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM atawaongelea.


Samwel ametoa ushuhuda wake mwingine wa kuwepo kwenye hiyo dini ya kishetani kwenye NJIA PANDA ya CLOUDS FM,

ITAMBUE MAANA YA FREEMASONS,ALAMA ZAKE NA MADHUMUNI YAKE 1

Hi | 6:37:00 PM | | 4 Comments so far
UTANGULIZI
Yapo mambo mengi sana duniani ambayo huja na kupita.mengi huwa tunayaona mageni pale tunapo yaona kwa mara ya kwanza.mfano vazi la suruali kwa wanawake. 

Vazi hili miaka ya 80 halikuwepo hapa kwetu tanzania.miaka ya 90 vazi hili lilianza kutumika japo watumiaji walipata vipingamizi vingi sana kama kubakwa,kuzomewa,kutengwa, nk.watu hao walionekana katika jamii kama wasaliti wa mila.hata hivyo mpaka sasa jamii imekwisha kubali matokeo.

 HISTORIA KWA UFUPI

Freemason  ni shirika ambalo mambo yake ni siri kuu. Mimi nilifanya utafiki  kwenye mitandao, nikafatilia historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa mara kwenye makala za historia katika televisheni za magharibi pamoja na kuongea na watu waliofuatilia kwa karibu mambo yao.

Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.
Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.

1. Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times). 

Niliambiwa walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs). 

Niliambiwa wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.

2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k

3. Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.

3. Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani. Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki. 

Ndio maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama Jesuits.

Jesuit Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye elimu ya juu zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti ndani ya kanisa katoliki.

4.Kuhusu imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini Yesu na Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mabaya. alimfanyia hila Lucifer aonekane mbaya.

4.Kinachoendelea ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna daraja ambazo muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea katika imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya juu kabisa ni nyuzi ya 33 (33rd degree)

5. Kwa hiyo ijapokuwa wanatumia biblia wanapoongelea “Bwana” huwa hawamaanishi Yesu bali huwa wanamaanisha Lucifer ambaye ndiye wanayemwabudu.

6. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi. 

Wafuasi wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini manake hata wao hawaambiwi kitu. Kwa wafuasi wa daraja ya chini wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa wasio jua kitu kule kwenye lodge zao ni kama ywca au wmca au club hivi. Kwenye nchi kama marekani watu wasio jua siri wanachukulia kama sehemu za kusocialize tu.

7. Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri, yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya utawala.

WALIOSHIRIKI KUPINGA  FREEMASON NA UASI WA
LIONS CLUB NA ROTERY CLUB

Kanisa la Katholiki wakati moja waliwahusisha Rotarians (Lions Club) moja kwa moja na Freemasons. Mwaka wa 1928 Maaskofu wa kihispania walitangaza wazi kwamba Rotary Club si chama tu cha kawaida bali ni Muungano au chama kipya cha kuabudu mashetani wakiwa na katiba, tabia na kila kitu chao kufanana na zile za Freemasons wakawatahadharisha waumini wao wajichunge sana na Chama hicho, na baada ya muda mfupi wakuu wa Vatican walitoa amri kwamba maaskofu wa kanisa la katoliki hawaruhusiwi kujiunga na vyama hivyo (Rotary, Lions Club).

Mohammed Sayed Tantawi
Katika miaka ya 1970 kiongozi wa juu na Sheikh wa Chuo kikuu cha kiisilamu huko Misri (Egypt) inasemekana alitoa fatwa kuwakataza waisilamu wasijiunge na chama cha Rotary Club na wakati mambo haya yalikua yakikatazwa na dhehebu la sunni Chama cha rotary pia kilisikika kukatazwa na Ayatollah Khomeini. 

Ayatollah Khomeini
katika mwaka wa 1798 Mwandishi Mmoja wa Kiingereza aliejulikana kwa jina la john Robbinson aliandika kitabu kijulikanacho kama Proofs of a Conspiracy Against All the Religions and Governments of Europe, Carried On in the Secret Meetings of Free Masons, Illuminati, and Reading Societies (Uthibitisho wa njama dhidi ya Dini zote na Serikali zote za Ulaya ilipangwa katika mikutano ya siri ya Freemasons, Illuminati, na vyama vinginevyo vya Reading)
John Robbinson

Kitabu hicho kinaelezea Ari na hamasa za Freemason walivyokuwa wakipanga kisiri jinsi ya kupinduwa mipangilio mizuri ya Maisha (Serikali) na ndio waliosababisha mapinduzi nchini Marekani na Ufaransa.

Shuku za kuenea kwa Freemasons zilienea hadi kufikia miaka ya 1800 ambapo 
Rais Wa 13 Millard Fillmore wa Marekani
alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge la Marekani (Congress) kama mgombea aliyekuwa akipinga mambo ya Freemasons na akafikia kilele katika karne ya 20 (20th Century)

Sergiei Nilus Mwandishi Kitabu cha Protocol
Kitabu cha The Protocols of the Elders of Zion sio kuhusu mayahudi kutawala dunia lakini ni kuhusu njama za freemason wa kiyahudi kubadili mfumo wa dunia.

Hitler Reinhard Heydrich
Hitler alizungumzia kuhusu njama za Mayahudi-Bolshevik-Freemason na kiongozi mwingine wa Ujerumani kwa jina la Reinhard Heydrich aliunda kikosi maalum (Special Section SS) kuangamiza ushawishi wa freemason nchini Ujerumani.

Moqtada al-Sadr Al Hawza
Nchini Irak, Gazeti la Moqtada al-Sadr lijulikanalo kama Al Hawza lilichapisha picha ya George H.W. Bush na Bill Clinton na akaelezea kwamba ishara ya mikono yao ilikuwa ni alama ya waandamizi wa kizayoni na freemason, na kama walivyo Wakatoliki Waisilamu pia waliwahusisha wanchama wa Rotary moja kwa moja na Freemasons na kusema vyama vyote viwili ni laana. 

Rais Bush Rais Clinton
Freemasons wamehusika moja kwa moja katika jitihada za kutawala Mashariki ya kati jitahada ambazo zilibuni uhasama kati ya Mashariki ya Kati na Jumuiya ya Magharibi.
Freemason walitoa fursa ya wafanyabiashara kuunda mtandao mmoja, hii ni katika malengo ya wafanyabiashara wanachama wa Freemason wa Ulaya wafungue ofisi za Freemason nje ya nchi na kuwaalika wanainchi wa Ulaya kujiunga nao.

Kwa ujumla sio Wafanya biashara wa Wakiingereza au Mashariki ya kati ndio waliowengi tu kama anavyoeleza bwana Hamid Algar wa Berkeley ambaye ni Mwanachuoni maarufu duniani wa historia ya Kiisilamu:-

Hamid Algar
Freemason imeweza kuhudumika katika uisilamu tangu kijitambulisha kwa waisilamu katika karne ya 18 kama njia ya kukuza utawala wa fikra za wa Magharibi kisiasa na kimawazo; Mojawapo wa Ofisi za Freemason huko Istambul nchini Uturuki, ilikuwa na Balozi wa Uingereza kama mkuu


TUKUTANE KATIKA  SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI HILI.,
ASANTENI.

WAASISI WA FREEMASONS NCHINI TANZANIA NA KUENEA KWA FREEMASONS KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI 2

Hi | 6:15:00 PM | | Be first to comment
Januari 2005 nchini Isarel ‘walipata’ kiongozi mpya wa Freemasons, Chaim Henry Gehl, ambapo sherehe yao ilifanywa katika Hoteli ya Sheraton iliyopo Herzlia. 

Wageni walitokana Uingereza, Ujerumani,Uholanzi, Austria, Luxemborg,Romania,Italia,Bulgaria na China. Kiongozi huyo alikuwa akikabidhiwa madaraka kutoka kwa Sami Raphaeli, mhasibu mstaafu wa benki mstaafu wa hekalu la Caspi lenye namba 56 lililopo mjini Haifa. Huyu cheo chake cha utendaji mkubwa katika freemasons ni 33rd degree alichotunukiwa mwaka 2003.

Naam katika kuselebuka huko ndipo wakajigamba kwamba mnamo Oktoba 9, 2004 kulifanywa sherehe ya kutimiza miaka 100 ya Freemasons katika eneo la afrika mashariki. 

 Hapa kwetu Tanzania haikusemwa sana, ingawaje Jayantilal Kashavji Chande , au Sir Andy Chande katika mahojiano yake na mwandishi wa Ernest C. Ambali(The Guardian, Oktoba 8, 2004) haikuelezwa mahali patakapofanyiwa sherehe hizo.

Katika mahojiano yale Sir Andy Chande alieleza kuwa mgeni rasmi alikuwa Rais Benjamini Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa. Pia kulikuwapo na wafanyabiashara wakubwa,wanadiplomasia,mawaziri n.k 

Sir Andy Chande akiwa nchini India katika mji wa Chennai kuzindia hekalu lao East Star alieleza  kwamba ‘marais wawili wa kwanza wa Tanzania (hawakuwa freemasons) lakini walifahamu ni nini’. Je unahitaji akili gani kuwatambua marais wako? Unahitaji Mungu akuongezee ubongo gani ili utambue kuwa ni akina nani wanaozungumziwa? Ndiyo maana nasema tatizo siyo kasi uliyonayo bali kule uendako!

Tukubaliane, kuwa kwa kiasi Fulani inajionyesha ikulu zetu zimezingirwa na Freemasons. Na katika mahojiano hayo hakusemwi ni Dar es Salaam eneo gani ambao sherehe hiyo ilifanywa, lakini katika kumsimika Chaim Henry Gehl (kule Israel)ilitajwa Hoteli ya Royal Palm ambapo wageni 350 walihudhuria.

 Katika miaka hii 100(108) ikaelezwa kuwa Freemasons walianza kujenga hekalu lao la kwanza la Harmony namba 3084 mwaka 1904 mjini Zanzibar.

Katika uzinduzi wa jengo hilo Zanzibar inaelezwa Rais Theodore Roosecelt alikuwapo, Duke of York(ambaye baadaye alikuja kufahamika kama Mfalme George VI)na Duke of Connaugh na Strathean walikuwepo pia. 

Ukimsoma mwanahistoria Robert Muchembled(katika; A History of the Devil) ameorodhesha majina yenye kuabudiwa kwa ibada za kishetani lakini tunayathamini na kupofushwa nayo. Nami kwa matendo wanayoyatenda hapa duniani sina soni kusimamia hoja yangu kuwa ni ubatili mtupu waufanyao).

Naweka orodha ya mambo wanayojigamba Freemasons kujinasibu kwa miaka yao 100(108) ndani ya afrika mashariki huku wakibainisha kuwa makao makuu ya eneo zima ni barabara ya Nyerere, jijini Nairobi(soma;The Guardian, 0ktoba 8, 2004). Katika mahojiano hayo ndipo kukaorodheshwa ‘misaada’(ibilisi?), eti Kindwitwi Leprosy Centre(Utete), Mama Theresa Home for the children, shule ya vipofu(Pongwe, jijini Tanga), na Leprosy Projects (jijini Arusha).

Montessori School (jijini Mwanza), Mnazi Mmoja Hospitali (iliyopo Zanzibar), Missionaries of Charity, shule ya walemavu (Buguruni, jijini Dar es salaam), wamejenga madarasa shule ya msingi Kinondoni(Dar es salaam) na kutoa pauni za Uingereza 15,000 mnamo mwaka 1996 katika ajali ya Mv Bukoba. Ukiangalia ‘misaada’ yao unapumbazika kuwa ni hisani ya hali juu

Na tatizo kubwa linalotukabili, ni utegemezi ambao huzaa utumwa na kukengeuka akili zetu. Tunaishi huru mitaani lakini tupo gerezani, tunakwenda kasi sana lakini hatuangalii tunakokwenda, hatutaki kujua nini hiki tunachosaidiwa?

Ni mungu gani aliruhusu mashoga na wasagaji wasimame madhabauni/altareni? Naam ndivyo tunavyouvaa uovu, ndivyo yanakotakiwa Uganda Museven aliruhusu hali hiyo. Na wenyewe husingizia haki za kiraia au dini za kiraia, inaeleweka kuwa Marekani imejngwa na Freemasons kwani wanajieleza kwa mengi tu. Je nasi tuwe na akina Jack Straw wetu bungeni? Tuvuje jasho kwa kupitisha sheria za kuruhusu mashoga, wasagaji halafu tuseme mungu anaruhusu hayo?

VIGOGO  WA FREEMASONS  KATIKA  UKANDA  WA AFRIKA MASHARIKI  NA AFRIKA  KWA UJUMLA
Sir.Andy chande ajitokeza na kusema kuwa yeye ni mmoja wa freemason afrika mashariki .Pia hakuwa nyuma kuwataja viongozi wanaohusika kwenye chama hicho akiwemo rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa .

Pia alimtaja steven kanumba, msanii nguli hapa Tanzania,Baba Riz raisi wa Tz,lowassa,AY,Mr. Blue,na wengineo wengi. Pia hakusita kumtaja yoweri museveni raisi wa uganda,Obama raisi wa marekani,George Bush,Bill Clinton,George washington,Elizabeth malkia wa uingereza na wengineo wengi.

 Sir.Andy Chande alitaja yeye kwenye chama hicho ni Grand District Master akiwa amebobea kwa miaka 18 iliyopita.

Alipoulizwa makao yao makuu hapa Tanzania yapo wapi alijibu bila kusita "we are located at sokoine Drive behind kilimanjaro hotel here in Dar es salaam" (tunapatikana barabara ya sokoine nyuma ya hoteli ya kilimanjaro).

Pia Sir. Andy alisema wananyaraka zote za kumiliki jengo hilo toka serikalini. Aliongezea kuwa vikao vyao hufanyika kwa siri nyakati za usiku na mtu akishaingia kwenye chama hiko hatotoka tena

TUKUTANE  KATIKA SEHEMU YA TATU  AMBAPO   TUTAZUNGUMZIA  JUU YA MALENGO YA FREEMASONS NA UJIO WA "NEW WORLD ORDER"
ASANTENI

FREEMASON UKUMBI WA KWANZA KUTUMIWA NA BUNGE LA TANZANIA

Hi | 2:28:00 PM | | Be first to comment
Huu ndiyo ukumbi wa Freemason uliopo Dar es Salaam, ambao ndio wa kwanza kabisa kutumiwa na Bunge la Tanzania. 
Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam
  Ukumbi wa Arnatouglou, Dar es Salaam
 Ukumbi wa Pius Msekwa, Dodoma
 Ukumbi wa Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi, Dodoma

June 29, 2012

SOMA HISTORIA YA FREEMASON NA UFAHAMU IMEGAWANYIKA KATIKA NYAKATI KUU MBILI TOFAUTIE

Hi | 7:07:00 PM | | Be first to comment
Hizi ni baadhi ya alama za Freemason 

Historia ya Freemason imegawanyika katika Nyakati kuu mbili tofauti, Yaani Kabla na baada ya Grand Lodge of England on 24th June 1717. Baada ya kutengenezwa kwa Grand Lodge huko Uingereza ambazo zilikuwa maalumu kwa Freemason, Freemason walianza kuenea Duniani kote kwa kutengeneza Lodges za mtindo huohuo katika nchi nyingine, na sasa ikafika hadi Tanzania, Kabla ya ukoloni. Marekani ilifika Mwaka 1775.

Ningependa kuwapa kazi ambazo wao huwa wanazifanya na Tabia za watu hawa ambao wapo kwenye Dini hiyo ya Kishetani.

1. Kusaidia watu wote wenye matatizo mbali mbali, Mfano majanga kama kwetu hapa Gongolamboto, Mbagalia Mabomu, Mafuliko, Kuunguliwa Moto nakadhalika 

2. Kusaidia vituo vya watoto yatima, Kuandaa sikukuu au mikutano ya vilema na wamama wajane.

3. Wanatoa misaada ya kupata kazi na awakati mwingine facilities na njia mbadala za kupata kazi.


Tabia zao 
1. Kwanza ni wapole na wanyenyekevu sana kwa watu na hawapendi makundi yenye kujitoa kimbelembele.
2. Wengi wao ni matajiri na watu maarufu, na wenye Heshima kubwa sana kwenye nchi husika, na wafanyabiashara.

3.
Watu wanaopenda kujitolea kwa hali na mali katika jamii, ikitokea tatizo lolote la kitaifa.
4. Wanaopenda kuanzisha mifuko mbalimbali kwaajili ya jamii Fulani, Lengo ni kupata

5. Hawapendi ugomvi au machafuko ya aina yoyote, ni watu wa Amani.

6. Hutumia Ufreemason wao kupata wateja kwenye biashara zao, au kupata watu wengi kwenye majukwaa ya kisiasa kwa lengo la kushinda chaguzi mbalimbali, kwa wanamuziki Ili miziki yao ipendwe na kupata watu wengi kwenye shoo zao. Wachezaji kwa Fowadi waweze kushinda magoli wawapo kwenye mechi, na Waigizaji kazizao zipendwe na wao wawe na followers wengi.

June 21, 2012

FREEMASONS WAJITOKEZA NA KUFANYA MAHOJIANO KATIKA KIPINDI CHA LEO TENA CHA CLOUDS FM JIJINI DAR ES SALAAM

Hi | 8:36:00 PM | | Be first to comment
 Cheki Kiatu Cha Freemason huyu.
Freemason wa Kisukuma 

Katika Kipindi Cha Leo Tena Katika Radio Maarufu ya Clouds FM pamoja na kwenye Clouds TV wamejitokeza Watu wanaodai wao ni Freemasons na Kueleza Wanavyofanya kazi.
Watu hao ambao inaonekana hawakuwa wamejipanga kwenda kwenye Media Wameshindwa kujibu baadhi ya Maswali waliyokuwa wakiulizwa na Mtangazaji Zamaradi. Mara Kwa Mara watu hao Wamekuwa Wakikinzana katika Maelezo wanayotoa kuhusu Freemasons.
Katika moja ya Maelezo Yao wameeleza Kila Mtu ni Freemason akiwa Mkristo ama Muislam anaweza kuwa Freemason walijichanganya zaidi baada ya kuulizwa kama ndivyo basi hawa Jamaa hawana ibada, wakasema "Huwezi Kuwa Mroman, Kama Hauendi Kwenye Ibada Za Waromani, vivyo hivyo kila Freemason lazima aje kwenye Ibada".
Kumekuwa na Wimbi la Watu Wanaoibuka na Kudai kuwa na ufahamu wa Kutosha Kuhusu Freemasons. Mungu aisaidie Tanzania Mungu atuepushe na roho ya Ujinga na Kukataa Mafundisho Ya neno la Mungu.
Hawa ndio wataalam wa level ya u-DR waliokuwa leo kwenye Leo Tena Wakieleza U-Freemason Wao.

MTANZANIA WA KWANZA KUKIRI KUWA NI MWANACHAMA WA DINI INAYOABUDU MASHETANI IJULIKANAYO KAMA FREEMASON SEHEMU YA 2

Hi | 8:24:00 PM | | Be first to comment
 Sir Andy Chande
*Nimepata kutambua umuhimu wa mafunzo ya Freemason katika kujenga hisia za utuwema na ukweli kwake mtu wenyewe na kw abinadamu wenzake. Moyo wangu mawazo yangu na roho yangu, vyote vimeimarika kutokana na kushiriki kwangu katika Freemason

*Mwaka 1972 nikachukua hatua yangu ya kwanza kuelekea kwenye madaraka makubwa zaidi katika Freemason nilipochaguliwa Afrisa Mkuu wa Wilaya wa kufanya kazi na Makao makuu ya Freemason ya Mkoa kule Nairobi ambao wakati ule ulikuwa unasimamia makambi kiasi cha ishirini na manane katika Afrika nzima

*Freemason Tanzania wamesaidia kituo cha watu wenye ukoma cha kindiwi wilayani Utete; Kituo cha watoto cha Mama Theresa; shule  ya Vipofu ya Pongwe, mkoani Tanga; Kituo cha yatima cha Arusha, Hospitali ya Mnazi mmoja kula Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni.


Tangu miaka hiyo ya 1920 idadi ya  vikundi vya Mason nchini Tanzania na  Afrika Mashariki kwa ujumla imeendelea kuongezeka. Ogezeko  kama hilo hilo limejidhihirisha katika Asia, Marekani ya  kusini, na baadaye Ulaya ya Mashariki, baada ya kipindi kile cha kuingia kwa ukomanisti lakini kwingine kote hasa Ulaya ya Magharibi, Amerika ya  Kusini na Australia, idadi ya Wanachama wa Mason wamekuwa wakipungua polepole na kuacha pengo kubwa duniani kutoka milioni saba waliokuweko wakati wa vita kuu ya kwanza hadi kufikia milioni tano tu.

Hata hivyo mchango wanaodai kuutoa ndugu hao millioni tano, kwa Chama chao na kwa Jamii, ni mkubwa sana. Wanatoa misaada kila mwaka, kulingana na kazi zinazotekelezwa na vikundi vyao, kiasi cha dola milioni 400 za Marekani. Huku Tanganyika, baadaye Tanzania, walisaidia kituo cha watu wenye ukoma cha kindiwi wilayani Utete; Kituo cha watoto cha Mama Theresa; shule  ya Vipofu ya Pongwe, mkoani Tanga; Kituo cha yatima cha Arusha, Hospitali ya Mnazi mmoja kula Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni, ni machache tu kati ya miradi mingi iliyogharimiwa na vikundi vya Mason.

Kati ya miradi hiyo yote, ule wa Shule ya Buguruni ndio ninaouthamini sana moyoni mwangu; maana mimi ndiye mwandishi na mchangishaji mkuu wa fedha; mhamasishaji na mtetezi mbele ya Viongozi Wakuu kwa niaba ya shule hiyo kwa muda wa miaka thelathini iliyopita lakini bado pamoja na shughuli zote hizo za maana, kwa muda wote huo niliokuwa Mwanachama wa Freemason mara nyingi wale Wanachama wa Zamani wamenyanyaswa sana na magazeti ya  nchi za Magharibi.

Kutoka kuonekana kuwa Chama ambacho huruma na dhamiri zake katika kumwinua binadamu zinathaminiwa, kama ilivyokuwa katika kipindi kirefu cha karne za kumi na nane na kumi na tisa na mwanzo wa karne ya ishirini, sasa kimeporomoshwa hadhi kw amashambulizi makali ya magazeti yasiyokuw ana msaada, kiasi cha kuigeuza Freemason kuwa kama kivuli tu, kikundi cha wafitini cha ajabuajabu waliojaa hila!
 Sir Andy Chande kulia akiwa na Rais Benjamin Mkapa
 
Ili kuanza kukielewa vizuri zaidi Chama hiki, na hivyo pengine kuanza kuoanisha dhana na hali halisi, lazima mtu arudi kwenye misingi Freemason itikadi yenyewe ya Wema na maadili ndiyo ilivyonitumbukiza katika mazungumzo yangu ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya 1950 na akina Campbell Ritchie na Maclean, juu ya huruma kwa binadamu. Wakati ule ndipo nilipoanza kutambua kuwa, kumbe, maana kamili ya Uanachama wa Freemason ni Sayansi ya Maisha ambayo lengo lake ni kumtia moyo mwanadamu kwa  kumwelekeza vile anavyotarajiwa kuwa mtu mwenye ukamilifu katika vyote.

Sehemu kubwa ya hoja hiyo ya Ukamilifu wa mtu inafichwa katika dhana, na       pengine ndiyo maelezo ya uvumi unaoelekezwa kwenye shughuli za Freemason. Lakini taratibu hizo zimejengwa kwa malengo ya makusudi, ambayo mimi nayaona kuwa mazuri tu, ya kuamua na kuboresha fikra, moyo na hadhi ya binadamu kwa hiyo katika hatua ya kwanza ya kuingizwa kwenye Freemason, mising mkuu ya maadili ya kusema kweli inayojenga Freemason inasisitizwa kiasi cha kutosha katika mawazo ya mtu anayetaka kujiunga na Chama au mtahiniwa.

Hatua ya pili ya Freemason inasisitiza kuendelezwa kwa vipaji na ufundi katika sanaa na sayansi ili mtu aweze kuwa na manufaa makubwa kadiri inavyowezekana katika maisha. Hatua ya tatu inatoa nafasi kwa mtu kufikiria saa chache za mwisho wa maisha yake, lau kama hili litaonekana kuwa kama ndoto kwa njia hivyo, huyo anayetaka kujiunga na Freemason anaelekezwa namna ya kuishi kwa kutumia nafasi zote kabisa zilizopo katika namna inavyooana na misingi mitatu ya Freemason, ambayo ni: Upendo wa kindugu, misaada na ukweli, na kwamba kifo ni lazima.

Misingi ni mitatu ikisha kufafanuliwa katika malekezo ya wakufunzi yanayositiri mengi kati ya matunda ya Freemason, ndiyo ilivyovutia zaidi nilipopata kujua kwa ndani, kwa mara ya kwanza, baadhi ya mambo katika kikosi cha Antient. Katika taratibu za Freemason, mzingi wa upendo wa kindugu unawaelekeza ndugu zetu wote kuwatambua  binadamu wote kuwa familia moja iliyoumbwa na huyo Mwenyezi, lakini wakati huo “msaada” unatoa ujumbe kuelekeza imani niliyofunzwa na baba yangu, yaani kuwasaidia  wenye shida iwe katika kuwapunguzia umasikini, au kuwaliwaza wanaosumbuliwa na matatizo. Huo ni wajibu wetu sisi sote.

“Ukweli”, msingi wa tatu nap engine, ndio muhimu kuliko yote ni dhana takatifu ambayo, kwa mwanachama wa Freemason, ndio msingi wa kila jema la binadamu “kuwa mtu mwema na kweli” ni somo linalotolewa mapema kwa kila mtu anayetaka kuingia katika Freemason; hivyo ni kauli inayotumiwa kila mahali kama zana ya kurekebisha na, kama ikibidi kuelekeza njia ya maisha na vitendo vya mtu kulingana na masharti yale manne muhimu ya Freemason: kiasi, uvumilivu, busara na haki.

Na misingi yote hii, na maadili na umuhimu unaojumuisha siyo tu mafunzo ya falsafa za watu wa kale, kuanzia wagiriki, paka Budha, mpaka Zaroster. Lakini hata za dini zinazojulikana. Kinyume na propaganda zinazoenezwa za Mafashisti wa kiitaliano na wengine wengi zaidi ya  hao, Freemason si chombo cha dini wala vile vile, kinyume chake, hakipingi dini; kwa kweli Freemason wanawakaribisha watu wote bila kujali imani zao za dini, wala hawafanyi mbinu za kubadili imani zao wala kuelekeza ibada zao; wanachojaribu tu ni kuwafanya binadamu bora zaidi.
Sir Andy Chande akiwa na wenzake wakipanda Miti jijini Tanga kama moja ya shughuli zao za kijamii.
 
Hivyo hiyo ndiyo dunia niliyoitumbukia mwaka 1954, na ikawa sehemu muhimu ya maisha yangu kuanzia hapo. Katika kipindi hicho nimepata bahati ya kushuhudia kujitolea kwa Wanachama wa Freemason katika kuwasaidia wenye shida ndani ya Afrika Mashariki na hata nje ya hapo. Nimepata kutambua umuhimu wa mafunzo ya Freemason katika kujenga hisia za utuwema na ukweli kwake mtu wenyewe na kw abinadamu wenzake. Moyo wangu mawazo yangu na roho yangu, vyote vimeimarika kutokana na kushiriki kwangu katika Freemason; na kuimarika huko kunatofautiana kabisa na hisia zinazotangazwa katika magazeti mashuhuri ya nchi za magaribi. Kuwasaidia wenzetu kuwasaidia wengine ndiyo misingi niliyojifunza katika miaka yangu mingi ndani ya Freemason.

Baada ya kushika nafasi za juu zaidi katika kambi hii ya Nyota ya Jaha mnamo miaka ya mwisho wa 1950 na 1960 nikateuliwa kuwa kiongozi mstahiki mwaka 1967, wakati huo ndio kwanza nimeteuliwa Rais wa Muungano wa vyama vya Round Table vya Afrika  Mashariki. Mwaka uliofuata, kwa vile nilivyokuwa Mwanachama wa kwanza wa Round Table asiyekuwa Mzungu, nikawa raisi wa kwanza wa Roundi Table na vyama vinavyoambatana nayo duniani mwenye asili isiyokuwa ya kizungu: ukweli ulioinua hadhi ya nafasi hii kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko ilivyokuwa  kawaida.

Kwa nafasi hiyo nikalazimika kusafiri sana, kuandamwa na Magazeti, na kuwa na shughuli nyingi za uwakilishaji kimataifa, mwaka 1970 nikakamilisha kipindi changu cha uongozi kama rais wa Kimataifa wa Baraza la Dunia la Klabu ya Huduma za Vijana; na mwaka uliofuata, baada ya kulazimika kustaafu kutoka katika chombo hicho kwa sababu ya umri, nikiwa makamu wa kudumu (wa heshima) wa Mwenyekiti wa Muungano wa Round Table katika Afrika Mashariki mwaka 1970 nikajiunga na Round Table ya Dar es salaam, hatua ya kwanza kuelekea kwenye nafasi ya Gavana aliyewajibika na klabu sabini na nane katika sehemu kubwa ya Afrika.

Mwaka 1972 nikachukua hatua yangu ya kwanza kuelekea kwenye madaraka makubwa zaidi katika Freemason nilipochaguliwa Afrisa Mkuu wa Wilaya wa kufanya kazi na Makao makuu ya Freemason ya Mkoa kule Nairobi ambao wakati ule ulikuwa unasimamia makambi kiasi cha ishirini na manane katika Afrika nzima.

Kila nilivyopata madaraka makubwa zaidi, ndivyo nilvyohakikisha kwamba nilifanya kila lililowezekana kutakasa Freemason mbele ya Umma. Kwa uzoefu wangu mimi, watu kwa kawaida hutilia mashaka, na hata kuogopa, mambo wasiyoyaelewa. Kwa hiyo wakati wote nilipoulizwa habari za Freemason nikajitahidi kumweleza huyo muulizaji misingi ya chombo hicyo, nikisisitiza kwamba hakikuwa chama cha siri, na wanachama wake wanajulikana wazi: na kwamba mikutano yake haifanyiki katika sehemu za kujificha ila katika kumbi za mikutano zinazojulikana, zenye hati ya serikali na zinazoweza kutambulika wazi wazi.

Kama nilivyokwisha kusema mapema chama hiki na maajabu yake, kiliingia wakati wa Vita Vikuu vya pili, tulipokuwa tunajaribu kuwalinda wanachama wetu waliokuwa Italia, ufaransa na Ujerumani dhidi ya vituko vya mataifa makubwa toka wakati huo tumejidhihirisha wazi wazi mbele ya umma, na kujitahidi wakati wote kuwaondolea mashaka na kudhihirisha kuwa chama chetu ni chombo kinachomwingiza mtu mwema na kujitahidi kumfanya mwema zaidi.Habari yote hii ni kwa Mujibu wa kitabu cha Sir Andy Chande

MTANZANIA WA KWANZA KUKIRI KUWA NI MWANACHAMA WA DINI INAYOABUDU MASHETANI IJULIKANAYO KAMA FREEMASON

Hi | 8:19:00 PM | | Be first to comment
 Jengo la Freemasons lililoko maeneo ya Posta jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akiwa na Sir Andy Chand
~ “Nilipoanza kutafuta uanachama wa Freemason nililazimika kutambua kuwa nilikuwa natumbukia katika mazingira ambayo sikuwa nayajua, ya kujitenga na dunia.”

 ~ Asema “Nina hati “takatifu” ya kuhani mkuu freemason”

~ kambi ya kwanza ya Afrika Mashariki ilianzishwa Zanzibar mwaka 1904

Sir Andy Chande ni mtanzania wa kwanza kukiri kuwa ni mwanachama wa kundi la Freemasons, Chande tofauti na kuwa member wa kundi hilo pia anakiri kuwa ameshika nyadhifa nyingi ndani ya kundi hili ikiwa ni pamoja na kutunukiwa hati takatifu ya Kuhani Mkuu. Katika maelezo yake pia ametaja asasi zilizofadhiliwa na kundi hilo lililoenea duniani kote.

Maisha yake kama mwanachama wa kundi hilo ameyaweka katika kkitabu chake Katika alichokiita  SHUJAA KATIKA AFRIKA, safari kutoka Bukene, Mzee Chande ni Mtanzania aliyewahi kushika nyazifa mbali mbali katika utumishi wa umma katika Serikali ya Tanzania  na kujizolea sifa kadhaa ikiwa ni pamoja na Heshima ya “Sir” aliyopewa na Malkia wa Uingereza. Katika kitabu hicho ameeleza kwa kina jinsi alivyoingia katika chama hicho Oktoba 25, mwaka 1954, akianzia na kambi inayoitwa Jaha iliyomaanisha kundi la watu wa daraja la nne.

Kati ya mwaka 1967 na 2003 Sir Andy Chande amekuwa mwenyekiti wa Tanzania Tourist Corporation, Tanganyika Standard Newspapers Ltd, East African Harbours Corporation, East African Railways Corporation and Cargo Handling Company of East Africa ltd.Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika mashariki Sir Chande alikuwa mwenyekiti wa Air Tanzania Corporation na baadaye akafanya kazi kama Mwenyekiti Mamlaka ya Bandari Tanzania na pia Mwenyekiti wa Tanzania Railways Corporation.

Katika Ukurasa wa 168 wa kitabu hiki kilichozinduliwa kwa heshima na viongozi wa wakuu wa serikali ya Tanzania, Sir Chande anasema:
“Kuwa mwanachama wa Freemason maana yake ni mtu kujitolea kuingia katika safari ndefu isiyo na mwisho ya kujifunza na kuchunguza. Kwa muda wa miaka 50 iliyopita mafunzo yangu ndani ya Freemason yaniwezesha kupata shahada nyingi za ngazi na umuhimu unaozidiana, ukiacha ukuu wa Wilaya nzima ya Afrika Mashariki, yaani Kenya  Sheli Sheli, Tanzania na Uganda, kwa miaka 19. Nikitaja nafasi chache tu nilizoshika, nimekuwa msimamizi wa kwanza mdogo kasha mkubwa wa kambi kuu ya viongozi wa Freemasons wa Uingereza na Wiles.

Mara ya kwanza kabisa nafasi hiyo kushikwa na mtu asiye mkazi wa Uingereza. Nimepewa heshima ya kuwa mstahiki kamanda wa kambi ya  Donyo sabuki ya royal Ark Mariner na nimeshika uongozi wa kambi hiyo toka mwaka 1990.

Mimi ni msimamizi mkuu wa Afrika mashariki wa kikosi kikuu cha Freemason cha Royal Ark cha Uingereza, nikiwa nimeshika nafasi hiyo tangu mwaka 1980, na ofisi ya wilaya tangu mwaka 1972. Mwaka 2000 nikawa Naibu Mshika upanga mkuu wa kikosi kikuu, nab ado mimi ni mkufunzi mkuu wa heshma katika kikosi kikuu cha Uskochi.

Mwaka 1987 nilipata shahada ya Mtakatifu Lawrence, shahidi; Shada ya shujaa wa Constantinople hati takatifu ya Kuhani Mkuu na Wawekezaji wakuu wa Suleiman; nikapata vilevile hati muhimu ya ushujaa ya msalaba mwekundu wa babeli mwaka 1988, nikaingia katika halmashauri ya wasimazimi wakuu namba 1, walioteuliwa na waliokuwa hodari mno nchini Uingereza na Wales, na nikapewa shahada ya  msimamizi bora kuliko wengine wote.  Mwakauliofuata nikaingia kama mwanafunzi wa mkataba katika jamii ya waabudu wa Freemasons, tawi la Row Assemblege”.

Katika maelezo ya Sir Chande hapo juu kama yaliyonukuliwa  katika kitabu chake hicho chenye kuheshimiwa sana nchini napengine hata duniani, yapo mambo mawili yenye kuhitaji udadavuzi makini zaidi. Mambo hayo ni mafunzo ya matambiko na jamii ya waabudu wa Freemasons.

Hata hivyo katika maelezo ya awali Sir Chande anasema chama hicho sio dini na wala hakiingilii dini ya mtu, wala hakimkatazi mwanachama wake kuabudu dini nyingine.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa chapisho la Kiswahili la kitabu hicho lilizinduliwa katika hafla kubwa iliyohudhuriwa na viongozi wakuu wan chi marais wastafu, mabalozi na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Shaaban Robert, Agosti 10, mwaka 2007.

Maneno yaliyopo kwenye hotuba ya Rais kikwete wakati wa uzinduzi wa kitabu hiki yanadhihirisha upekee na umuhimu wake na hata kile kilichomo ambacho wengi hawakijui. Rais katika sehemu ya hotuba hiyo alisema:

“….Aidha, napenda kukupongeza kwa dhati kwa kitendo chako cha kuandika kitabu hiki kinachohusu maisha yako. Sote  tunatambua kuwa kuandika kitabu sio kazi rahisi hata kidogo. Ni jambo linalohitaji ujasiri, umakini, nidhamu na uwezo wa hali ya juu.  Hivyo kwa  kuandika kitabu hiki  kinachogusia maisha yako kwa kipindi kinachozidi miaka 77 umeonyesha wazi kipaji na uwezo mkubwa ulio nao. Si watu wengi walio na uwezo kama ulionao wewe. Tunakupongeza sana.

Lakini kubwa zaidi nakupongeza kwa kuandika kitabu hiki kwa umakini na ufasaha mkubwa. Umeweza kwa kiwango cha hali ya juu kueleza mazingira halisi ya hali ya nchi yetu ulimokulia,  kufanyia kazi na sasa unamozeekea. Kitabu chako ni mchango mkubwa kwa historia ya nchi yetu ambayo tunauenzi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Nawaomba watanzania wenzangu wakisome kitabu hiki kila watakapopata nafasi, ninahakika watafaidika sana na kile watakachokisoma. Ingekuwa  jambo jema sana maktaba za shule na vyuo vyetu vikawa na nakala ya kitabu hiki, hivyo kuwawezesha vijana wetu kufahamu kwa undani zaidi historia ya nchi yetu na watu wake kwa ujumla”
Lakini hofu kubwa kwa jamii  isiyofahamu vyema mambo hayo ni kuwepo kwa neno kuabudu ambalo tafsiri rahisi ni Tafsiri hahisi ya Neno Matambiko lililopo katika maelezo binafsi ya Sir Chande. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu ni: Utekelezaji wa ada maalumu ili kutuliza mizimu, au pepo, edah, kafara, mviga mviko.

Tafsiri ya Neno kuabudu ni: “kufanya ibada, kuheshimu kwa hali ya juu unyenyekevu wa hali ya ju. Aidha tafsiri nyingine zaidi ni tendo linaloambatana na  kutoa sadaka.

Akieleza safari yake jinsi alivyojiunga na kundi hilo Sir Chande alisema.

“Nilipoanza kutafuta uanachama wa Freemason nililazimika kutambu kuwa nilikuwa natumbukia katika mazingira ambayo sikuwa nayajua, ya kujitenga na dunia. Maana ingawa mpaka wakati huo Chama cha Freemason kilikuwa katika sura hiyo hiyo kwa karibu miaka mia  tatu (Kambi hizo mbili ziliunganishwa uingereza mwaka 1715), hali ya usirisiri wake unaokigubika imeongezeka sana katika miaka hii michache.

Freemason walikuwako katika sehemu yangu hii ya dunia kwa muda wa miaka hamsini, kambi ya kwanza ya Afrika Mashariki ikiwa imeanzishwa Zanzibar mwaka 1904, lakini ikichukua miaka mingine ishirini na minne kwa kambi ya kwanza ambayo, kwa shamra nyingi, Gavana ndiye aliyeiwekea jiwe la msingi ili ijengwe huko Bara katika Mtaa ulioitwa wakati ule; Main Avenue, sasa hivi Sokoine.

April 22, 2012

MAREHEMU STEVEN KANUMBA ALIKUWA FREEMASON?GAZETI LA NYAKATI LIMEANDIKA

Hi | 5:44:00 PM | | 5 Comments so far
Nilipoandika wiki inayoisha leo juu ya imani na ujinga juu ya Freemason hakika kumbe sikujua ukubwa wa tatizo.nimepokea simu nyingi na meseji zaidi ya 200 kati ya hizo wengi wakionekana kusema mimi ndiye mjinga ninayepingana na ukweli kuwa Freemason hawapo.Lakini mimi sikusema hawapo,ila nilisema tunachosema kuwahusu ndiyo ujinga kwani tunawasingizia na kujitia hofu juu ya ujinga wetu wenyewe kutokuwa na imani na kutopenda kusoma wala kijifunza ila kuishi kwa majungu,uzandiki na unafiki wa hali ya juu huku tukijifanya ni waumini wa dini.
Leo gazeti linalojiita la kikristo linachapisha habari tena ukurasa wa mbele juu ya Kanumba kuwa freemason.nimezoea kuona mambo hayo kwenye magazeti ya udaku.kwa hiyo kwangu mimi hili nalo ni gazeti la udaku.sina ugomvi na kanumba kuwa mwanachama wa freemason(kama alikuwa kweli,kwani ni haki yake kujiunga na kundi lolote lisilovunja katiba na sheria za nchi),Lakini gazeti la kikristo lilipaswa kujua ujinga ulioenezwa hata na baadhi ya madhehebu ya kikristo juu ya Freemasons tena dhidi ya ukristo na kujua athari ya habari ya kijinga kama hii kuwa katika gazeti la kikristo,mathalani Nyakati hawaonyeshi kadi ya uanachama wa kanumba kwenye chama hiki,wala halisemi alianza mafunzo kwenye lodge ipi wala ni lini na wapi alijitambulisha kama freemason.Nimeshasema na nirudia tena ni UJINGA kukusanya michoro kwenye nguo ya mtu au mapambo anayovaa kama lilivyofanya Nyakati eti ndiyo ushahidi kuwa mtu fulani ni Freemason.mimi nimeona kwa macho yangu mwenyewe wachungaji wengi wakati wa mahubiri tena wakiwa mimbari wakijishika tumboni wakati wanaongea.naam nimewaona akina mwakasege,mzee wa upako,gwajima,lwakatare,nimewaona akina askofu kulola,kakobe,askofu pengo,malasusa,mokiwa,nimewaona waandishi wa habari,wahadhiri,nimewaona wazazi wangu,naam hata mimi hujishika tumboni ninapoongea.kwa mujibu wa Gazeti la kikristo la Nyakati sisi wote ni Freemason,jamani huu ni UPUMBAVU Fullstop.
Hebu niongeze:yeyote ajitazame vizuri,kama umevaa chupi,kama ukivaa suruali unavaa na mkanda,kama unavaa pete ya ndoa au ya urembo,bangili,kama unanunua bidhaa supermarket,kama unamiliki gari,baiskeli,kama unatibiwa kwenye hospitali kubwa,unasali makanisani,misikitini(kote huko freemason wametawala),kama unavaa tai,koti,viatu,wewe ni freemason tuuu.Naendelea jitazame unapotembea unaanza kwa kutumia mguu wa kulia,unajisaidia haja kubwa kwa kuchuchumaa au kukaa,haya ukipiga muayo unafunika kinywa kwa kitambaa ni freemason wewe,unaweka hela kwenye waleti au pochi,unakunywa soda za koka,maji ya kilimanjaro wewe tayari ni freemason,naam mwanamke umeolewa na unalala ukutani (freemason hawalali karibu na ukuta),haya twende unatumia kipaza sauti kuongea(vifaa vya freemason),unakula nyama ayayayayaya! ndo freemason mkubwa.Jamani hebu tuache UJINGA HUU.
Hivi sisi waafrika tunajidhalilisha? wakoloni walipotuita nyani kasoro mkia haikutosha? tulipoitwa chimpanzee haikutosha? sasa mbona tunatiana hofu zisizo na kichwa wala miguu?eti freemason hawaamini mungu? nani kasema? eti wanauwa watu kwa nguvu za giza! jamani kweli sisi mbumbumbu mzungu wa reli.
zamani tuliwasingizia wazungu kwa udhalili wetu,lakini leo tunaouhuru angalau wa bendera,wengine tumehesabu madirisha ya shule hadi vyuo vya nje,lakini bado tunazungumza ujinga,kwa nini wazungu hawana huu ujinga?sisi mbona tunajidumaza wenyewe? kwa nini tunaunga mkono kwa vitendo tuhuma kwamba sisi tumelaaniwa?
Nimalizie kwa namna ya mwaliko kwa makanisa kwani naona kuna hitaji maalum kufanya hivyo.Huko nyuma ukristo umewahi kuitwa Bangi( An opium of the people),Ni hivi ili kuzuia usanii,shughuli za uongo na mwenendo wa hovyo katika kukabiliana na matatizo ya watu wa siku hizi tunahitaji wachungaji,maaskofu,na wahubiri wasomi walosjifunza wakafunzika elimu mbalimbali ili wafundishe kwa utulivu wakitumia vichwa badala ya matumbo kama wengi wanavyofanya sasa,eti mtu akiweweseka kidogo wanakimbilia kusema eti ni mashetani,mara majini,mara laana za mizimu hivyo anahitaji kuombewa na kadhalika,huku ni kufanya mambo ya kienyeji kuliko hata wapiga ramli.Hali holela kama hii inatia aibu na kinyaa kanisa letu la kristo na inaunga mkono kwamba ukristo ni bangi,wakati kanisa tangu mwanzo lilikuwa kiongozi kwenye elimu ya kisasa.
Basi tunawahitaji viongozi wa dini wasomi watakaoweza kubaini kwa uhakika ugonjwa upi ni ugonjwa wa kimwili,upi wa kisaikosomatiki na upi ni wa kupagawa na shetani kweli.Wachungaji wa hivyowasomi wa kweli watatuepushia kiu holela ya utendaji miujiza na hivyo kutuepusha na aibu mbaya ya kuonekana wasanii na matapeli wa imani.si vyema kanisa kujihusisha na uwongo utakaomtukanisha roho mtakatifu
Jamani kama hamniungi mkono katika hili,basi peke yangu nitabaki maana sitaki kuona mtu anadanganya kama walivyofanya gazeti la nyakati nami nikaa kimya.Msidhani nimehama mada,hapana naongelea UJINGA wa hofu wa freemasons na wahusika wakuu wa kusambaza hofu hiyo ni wahubiri uchwara wanaowatia watu hofu na sasa gazeti la kikristo linaunga mkono ushirikina.si mmesikia injili za siku hizi zinavyohubiri mafanikio na kwamba mkristo hapaswi kuteseka hata kidogo? huu nao ni upotofu na danganya toto,habari za mtu kufufua misukule,habari za kuponya wagonjwa holela kwa miujiza,na ujinga mwingine,ndivyo vinavyokoleza hata huu juu ya freemason,SHETANI anaonyeshwa kuwa na nguvu juu ya Mungu,badala ya kuhubiri shetani na woga hubirini juu ya nguvu ya neema na ushindi wa mkristo na kristo dhidi ya shetani.
Gazeti la nyakati limetia aibu ya milenia.
LUDOVICK
0715 927100: 0753 927100

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster