Showing posts with label AIRTEL. Show all posts
Showing posts with label AIRTEL. Show all posts

December 15, 2013

AIRTEL YAWAJENGEA UWEZO WATANGAZAJI WA RADIO

Hi | 7:46:00 PM | | Be first to comment
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akisistiza jambo kwa watangazaji wa vipindi vya redio mbalimbali (hawapo pichani) kuhusu vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni bingwa" itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.Kulia kwake ni ofisa wa matangazo wa Airtel Bw. Abdallah Gunda.

August 6, 2013

MSHINDI WA KWANZA KWENYE SHINDANO LA NYUMBA AIRTEL YATOSHA APATIKANA

Hi | 6:13:00 PM | | | Be first to comment
Airtel Tanzania leo imetangaza mshindi wa kwanza wa nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha Shinda nyumba inayoendelea na kuwazawadia wateja wake kila siku.

Bwana Silvanus Juma mkazi wa Iringa mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni mhasibu katika shirila la Tanzania Rural women and children development foundation - TARWOC ameibuka mshindi na kuzawadiwa nyumba kisasa iliyojengwa na shirika na nyumba la taifa NHC iliyopo kigamboni jijini Dar es saalam.

July 17, 2013

DROO YA KWANZA YA PROMOSHENI YA AIRTEL YATOSHA INAVYOCHAGUA MSHINDI WA KILA SIKU

Hi | 7:08:00 PM | | | Be first to comment
Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akionyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) jinsi droo ya Airtel Yatosha inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya   promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya ashindi 7 ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.

July 4, 2013

BREAKING NEWS..! KILA MTANZANIA ANAYEMILIKI SIMU YA MKONONI UTALIPA KODI YA SERIKALI TSH . 1000 KUPITIA LINE YAKO

Hi | 10:25:00 PM | | | | | | Be first to comment
Kila mtanzania anayemiliki simu ya mkononi utalipa kodi ya Tshs 1000/= kwa mwezi kwa kila kadi (laini) ya simu uliyonayo na hii  imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na imeanza rasmi sasa, Kiasi hicho cha pesa unalipa wewe mwenye line na kampuni yako itakusanya kwa niaba ya serikali.

May 24, 2013

AIRTEL YATOA OFA KUPIGA SIMU KWENDA NJE KWA GHARAMA NAFUU ZAIDI

Hi | 11:58:00 PM | | | Be first to comment
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kushoto) na Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo (wa pili kutoka kulia) wakizindua huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine ni Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampun hiyo, Sunil Colaso.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice  Singano (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine   wanaofuatia ni Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Sunil Colaso na Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kutoka kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine ni Meneja Biashara  za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo (kulia), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Beatrice Singano na Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw.
Airtel yazindua ofa kabambe kupiga simu kwenda nje ya nchi

• Wateja kupata kifurushi cha dakika 25 kupiga simu kwenda India
• Ofa hii inapatikana masaa 24 siku 7 za wiki,

Kampuni ya Bharti (“Airtel”) inayoongeza kwa kutoa huduma za mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na Asia leo imetangaza uzinduzi wa ofa itakayo wawezesha wateja wa Airtel Tanzania kupiga simu kwenda nje kwa gharam nafuu zaidi.

AIRTEL YATOSHA LONGA NA WALIO INDIA KWA BEI NAFUU, KWA TSH 3000 TU DAKIKA 25 WIKI NZIMA.

Hi | 11:41:00 PM | | | | | Be first to comment
Sasa Airtel ya kuwezesha kulonga zaidi na walio india kwa bei nafuu, Kwa tsh 3000 tu utapata dakika 25, za kuwasiliana wiki nzima.

Kujiunga piga*149*13# upate kuwasiliana kwa bei poa ya shilingi 2 kwa sekunde.

May 16, 2013

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA IJULIKANAYO KAMA AIRTEL PREMIUM

Hi | 7:34:00 PM | | | | | Be first to comment
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Sunil Colaso akimzawadia  bi Rose Maina mmoja wa wateja katika uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam akifuatiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja bi Adriana Lyamba.
 Mteja wa Airtel bw. Picket Robert Miranda (kushoto) akiongea na mkurugenzi wa huduma kwa wateja Adriana Lyamba (kulia) na Meneja wa huduma kwa wateja Hilda Nakajumo (katikati)  katika uzinduzi wa huduma mpya ya wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Adriana Lyamba akimzawadia  bw. Abdual Salum mmoja wa wateja katika uzinduzi wa huduma mpya ya wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam, akishuhudia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Airtel  Sunil Colaso.

April 15, 2013

AIRTEL YATOSHA BOFYA *149*99# KATIKA SIMU YAKO ILI KUFURAHIA MUDA WA MAONGEZI NA VIFURUSHI VYA INTERNET KWA GHARAMA NAFUU SANA

Hi | 2:50:00 PM | | | | | Be first to comment
Airtel yatosha furahia uhuru wa mawasiliano kwa kuchagua muda wa maongezi na vifurushi vya internet kwa gharama nafuu sana kwa kubofya *149*99# katika simu yako ya mkononi.
Nunua mda wa maongezi kwa siku na kifurushi cha internet
1. 349Tsh=Dak10+100Sms+25MB
2. 499Tsh=Dak25+200Sms+75MB
3. 749Tsh=Dak30+Sms Bila Kikomo+250MB
4. 999Tsh=Dak40+SMS Bila Kikomo+400MB
Nunua mda wa maongezi kwa wiki na kifurushi cha internet
1. 1999Tsh=Dak70+700Sms+175MB
2. 2999Tsh=Dak175+1400Sms+500MB
3. 4499Tsh=Dak210+Sms Bila Kikomo+1.5GB
4. 5999Tsh=Dak275+Sms Bila Kikomo+3G

March 6, 2013

AIRTEL “AMKA MILIONEA” ZAONGEZA ZAIDI YA MILION 270

Hi | 8:32:00 PM | | | Be first to comment
Airtel “AMKA MILIONEA” zaongeza zaidi ya Milion 270
·         Kwa siku 60  zaidi ya wateja 580  wa Airtel kuibuka na Mamilioni hayo
·         Tuma shinda kwenda 15595 ili kujiweka kwenye ushindi
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeongeza muda wa promosheni yake kabambe ya AMKA MILIONEA pamoja na sambamba na kuongeza kiasi kikubwa cha MPUNGA ili wateja wake kuendelea kujizolea mamilioni zaidi
 Meneja Uhusiano wa Airtel Bw. Jackson Mmbando ametuhabarisha kuwa promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90 hapo awali na kufanikiwa kuzawadia  zaidi ya milioni 400 kwa wateja wameamua kuiendeleza ili wateja waendelee kufaidi zaidi

January 31, 2013

VIWANGO VYA PUNGUZO LA KUPIGA SIMU KWA MITANDAO YA TZ, MARCH 2013, JAN 2014, 2015 NA 2016

Hi | 12:19:00 PM | | | | | | Be first to comment
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imeyataka makampuni ya simu za mkononi Tanzania kuhakikisha yanaanza rasmi mpango wa punguzo la bei ya kupiga simu katika mitandao mingine kutoka bei inayotumika sasa hivi ya shilingi 113 kwa dakika mpaka shilingi 34 na senti 92 ikiwa ni bei mpya inayotakiwa kuanza kutumika kuanzia siku ya kwanza ya mwezi March 2013.

Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA Profesa John Nkoma amesema uamuzi wa kufanya hivyo ni kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ambapo makampuni hayo yanatakiwa kuanza utekelezaji wa agizo hilo na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa kampuni yeyote ambayo itafanya kinyume na hayo maagizo.

Namkariri akisema “bei itaendelea kushuka kadri miaka inavyokwenda, tarehe 1 january 2014 bei itatakiwa kuwa sh 32 na senti 40, tarehe 1 january 2015 sh 30 na senti 58, tarehe 1 january 2016 itatakiwa kuwa sh 28 na senti 57, hizi bei ni za juu kabisa na Kampuni za simu ni ruksa kwao kuzungumza na wakatumia bei ya chini kabisa”

January 7, 2013

AIRTEL SASA KUTUMA SMS KWA SHILINGI MOJA

Hi | 2:06:00 AM | | | | Be first to comment
Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya SMS kichizi ambapo wateja wa Airtel sasa wanaweza kutuma sma kwa gharama ya shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, katikati ni Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami na kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami akionyesha kipeperushi cha huduma ya SMS kichizi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo itakayowawezesha wateja wa Airtel nchini kutuma ujumbe mfupi wa sms kwa shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde

December 13, 2012

TASWIRA ZA ONYESHO MAALUMU LA MUZIKI LA CHRISTMAS LA KWAYA YA DAR CHORAL SOCIETY LADHAMINIWA NA AIRTEL

Hi | 1:16:00 AM | | | | | 1 Comment so far
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor (katikati), akizungumza na mmoja wa wateja mashuhuri wa kampuni hiyo, Jaji Joaquine Antoinette De-Mello(kushoto) katika onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya ya Dar Choral Society lililodhaminiwa na Airtel katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Airtel. Irene Madeje.
 Kikundi cha kwaya cha Dar Choral Society kikitumbiza katika onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya hiyo lililoandaliwa na Airtel kwa wateja wao wa makampuni katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.
 Father x-mas akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto waliohudhuria onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya ya Dar Choral Society lililoandaliwa na Airtel kwa wateja wao wa makampuni katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya wanamuziki wa Kikundi cha kwaya cha Dar Choral Society wakionyesha umahiri wao katika onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya hiyo lililoandaliwa na Airtel kwa wateja wao wa makampuni katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Airtel, Irene Madeje (wa pili kushoto) akizungumza na baadhji ya wateja wokatika onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya ya Dar Choral Society lililoandaliwa na Airtel kwa wateja wao wa makampuni katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watu waliohudhuria onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya ya Dar Choral Society lililoandaliwa na Airtel kwa wateja wao wa makampuni katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa

December 7, 2012

AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI MPYA KWA AJILI YA WATEJA WAKE MWISHO WA MWAKA 2012

Hi | 3:58:00 PM | | | | | | Be first to comment
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Airtel "AMKA ILIONEA" kulia ni Meneja Huduma za Ziada Airtel, Francis Ndikumwami na Afisa Matukio wa Airtel kshoto, kujiunga na promosheni hiyo mteja atatakiwa kutuma neno SHINDA au WIN kwenda namba 15595 bure na atapokea maswali atakayoyajibu na kukatwa sh 350 kila sms na kupata pointi zitakazomuwezesha kushinda.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua promosheni mpya ili kuweza kuwazawadia wateja wake wakati wa msimu huu wa mwisho wa mwaka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo kwa waandishi wa habari Meneja wa huduma za ziada wa Airtel Francis Ndikumwami alisema kwamba "Airtel inakutoa fursa nyingine kwa Tanzania kushiriki na kushinda zawadi ya fedha taslimu wakati wa msimu huu wa sherehe.
Leo tunazinduzi "AMKA MILIONEA" amabazo jumla ya zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi milioni 401zitatolewa ndani ya siku 90 tu.
Kutakuwa na washindi wa kila siku, kila wiki, kila mwezi na zawadi kubwa moja itatolewa mwisho wa promosheni, katika promosheni hii wateja wa Airtel 875 watazawadia hizo milioni 401.

AMKA MILIONEA itakuwa na washindi wa aina tofauti tofauti . Washindi wa kila siku, kila wiki na kila mwezi, AMKA MILIONEA itahakikisha kila siku kunawashindi 10 kushinda kila siku na watagawana jumla ya shilingi 3,000.000, kila wiki jumla ya shilingi milioni 6,000,000 zitashindaniwa na washindi 10 na kila mwisho wa mwezi mshindi mmoja atashinda kitita cha shilingi milioni 30 wakati milioni 50, 0000Tshs itaenda kwa mshindi mmoja mwisho wa promosheni hii.
Akizungumza jinsi ya kujiunga na promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema, Ili mteja aweze kushiriki inabidi atume neno WIN/SHINDA kwenda namba 15595 bure na utakuwa ujiungajiunga, Baada kujiunga mteja atakuwa atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata maswali ambayo atajibu na akipata sahihi atapata ponti 20 akikosea atapata ponti 10. Na kwakila ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha shilingi 350 pamoja na kodi.
Amka milionea imeanza leo Desemba 3, 2012 itaenda hadi Machi 2, 2013.
Vigezo Muhimu
Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 ya kwa zawadi ya kila siku .
Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 yakwa zawadi ya kila wiki
Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 zawadi ya kila mwezi.
Mshiriki mmoja unaweza kushinda mara moja zawadi ya kila siku, mara moja zawadi ya kila wiki na mara 1 zawadi ya kila mwezi. Lakini pia anaweza akajishindia zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni.

Kujiunga
Tuma neno "WIN / Shinda", kwenda namba 15595 ( bure), na kisha utapokea ujumbe wa ukaribisho utakaombatana na maswali utakayojibu.

Kila jibu sahihi mteja atapata pointi/alama 20 na akikosea atapata pointi 10 zitakazomuwezesha kushinda, ukijibu maswali mengi
unajiongezea nafasi ya ushindi.

October 22, 2012

Bharti Airtel becomes the fourth largest mobile operator in the world

Hi | 5:25:00 PM | | Be first to comment
If you cannot read that message, click here.
 

 
PRESS RELEASE
 
Bharti Airtel becomes the fourth largest mobile operator in the world
 
Over 250 million mobile subscribers
 
NAIROBI, Kenya, October 21, 2012/ -- Bharti Airtel (http://www.airtel.com), a leading telecommunications service provider with operations in 20 countries across South Asia and Africa moved up one notch in the world wide ranking to be the fourth largest mobile operator in the world in terms of subscribers. (Source: Wireless Intelligence ‘Scoreboard’).
 
 
Top Five Operators Globally:
 
Operator
Connections
(millions)*
YoY Growth,
connections
China Mobile
683.08
11 %
Vodafone Group
386.88
5 %
America Movil Group
251.83
7 %
Bharti Airtel
250.04
13 %
Telefonica Group
243.51
7 %
(Mobile operator worldwide group global ranking by connections, Q2 2012)
 
*Connections are aggregated as the sum of each group’s subsidiaries where a minimum of 50 % plus one share economic interest is held.
 
At the end of the quarter ended June 2012, the Company had over 250 million mobile subscribers across its operations, representing  13% Y-o-Y growth.
 
Bharti Airtel had become the fifth largest mobile operator in the world following its acquisition of Zain Group’s mobile operations across 15 African nations in June 2010.
 
Distributed by the African Press Organization on behalf of Bharti Airtel Limited.
 
For more details visit
 
 
About Bharti Airtel
    
Bharti Airtel Limited (http://www.airtel.com) is a leading global telecommunications company with operations in 20 countries across Asia and Africa. Headquartered in New Delhi, India, the company ranks amongst the top 5 mobile service providers globally in terms of subscribers. In India, the company's product offerings include 2G, 3G and 4G wireless services, mobile commerce, fixed line services, high speed DSL broadband, IPTV, DTH, enterprise services including national & international long distance services to carriers. In the rest of the geographies, it offers 2G, 3G wireless services and mobile commerce. Bharti Airtel had over 259 million customers across its operations at the end of September 2012. To know more please visit, http://www.airtel.com
SOURCE 
Bharti Airtel Limited

October 1, 2012

AIRTEL YASHEREHEKEA UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NA WATEJA WAKE

Hi | 7:46:00 PM | | | Be first to comment
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wa kitengo cha huduma kwa wateja wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam
Mmoja wa wateja akimlisha keki  Mkuu wa kitengo cha  huduma kwa wateja Adrian Lyamba wakati wa  uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam
Mfanyakazi wa huduma kwa wateja Atupiana Msuya  akigawa vinywaji kwa baadhi ya wateja waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam
 Mkuu wa kitengo cha  huduma kwa wateja Adrian Lyamba akimlisha keki moja ya wateja aliyetembelea katika duka la Airtel lilolopo Moroco jijini Dar es saalam wakatii wa ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja  ambapo Airtel imefungua wiki ya huduma kwa wateja wiki nzima kwa kusherehekea na kuwashukuru wateja wake nchi nzima.  Halfa hiyo imefanyika katika makao makuu ya Airtel jijiini  Dar es saalam
Wafanyakazi wa Airtel wakitoa huduma  ya internet kwa a wateja waliotembea katika duka la Airtel lilipo Moroco jijini Dar es saalm ambapo Airtel leo imesheherekea uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja na kuwashukuru wateja wake kwa kutumia huduma na mtandao wa Airtel

September 15, 2012

August 19, 2012

AIRTEL YATOA OFAKALI KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA BLACKBERRY

Hi | 3:33:00 PM | Be first to comment
Airtel Tanzania, waanzilishi wa huduma za Blackberry hapa Tanzania sasa wana ofa kali zaidi ya huduma za Blackberry Tanzania!
Sasa, Kwa Sh 3,500 TU kwa wiki utapata BBM, emails papo hapo, facebook, Twitter, kuperuzi internet ya 3.75G na zaidi!
Piga namba 148*77# kupitia simu yako ya Blackberry uchague kifurushi chako ufurahie dili poa zaidi ya Blackberry Tanzania, Kutoka airtel !

August 1, 2012

AIRTEL TANZANIA YAENDELEA KUSAMBAZA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA-MWANZA

Hi | 11:30:00 AM | Be first to comment
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh Charles Kitwanga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mawasiliano uliojengwa na Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, wakwanza kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando. hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.
Mtandao huo wa Airtel kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke.

Airtel Tanzania imezindua mtambo kabambe wa mawasilano katika mkoa wa kanda ya Ziwa nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ikiwa ni mkakati wa Airtel uliojiwekea katika kuendelea kufikisha huduma zao bora  vijijini.

Akizindua mnara huo mpya Naibu mwishoni mwa wiki Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Raisi Mhe, Charles Kitwanga (mawe matatu) amesema Maendeleo vijijini yatakuwakwa kasi sana iwapo wananchi watatumia mawasiliano ya simu za mkononi kutafuta masoko ya madini, mifugo au vyakula wanavyozalisha  sehemu mbalimbali.

Waziri Kitwanga alibainisha hayo katika kijiji cha Nyamayinza kata ya Gulumungu wilaya ya Misugwi Mkoani Mwanza wakati akiongea na wananchi na kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya Airtel Tanzania.

Alisema “Mawasiliano yanafaida kubwa sana duniani na ndio hufanya maendeleo ya jamii kwenda kwa kasi, hivyo wananchi wa vijiji vyote vinavyoizunguka nyamayinza tumieni fulsa ya kupata mawasiliano haya ya Airtel kwa kuendesha au kuendeleza biashara zenu,pia anzisheni biashara za kutuma na kupokea pesa za Airtel Money  na mtumie mawasiliano haya haya pia kutafuta wateja wakutosha katika bidhaa za kilimo na mifugo mnazozalisha”

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster