Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

September 18, 2013

FRANCIS CHEKA NAHITAJI KUWA MPYA KIELIMU ILI NIFIKE MBALI NAAMUA KUANZA KIDATO CHA KWANZA

Hi | 1:18:00 AM | | | Be first to comment
Bingwa wa dunia wa WBF Francis Cheka ambaye hivi karibuni alipewa zawadi ya  kiwanja na Rais Jakaya Kikwete baada ya ushindi wake dhidi ya bondia wa Marekani, ameamua kurudi shule.Cheka anasema hakupata nafasi ya kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba. “Mimi sikusoma niliishia darasa la saba, lakini nimeamua kurejea darasani baada ya kupewa udhamini na shule ya St Joseph”.

August 8, 2013

JUMA KASEJA NI NI MIONGONI MWA WADAU WATAKAOHUDHURIA FAINALI YA KOMBE LA MEYA JIJI LA MWANZA - MEYOR'S PEPSI CUP

Hi | 3:37:00 PM | | | Be first to comment

Na Mashaka Baltazar, Mwanza
BALOZI wa Pepsi, Juma Kaseja ni miongoni mwa wa wadau wa soka walioalikwa kushuhudia fainali ya kuwania kombe la Meya wa Jiji la Mwanza (Meyor’s Pepsi Cup ), Stanslaus Mabula.
Mlinda mlango huyo namba moja wa timu ya taifa (Taifa Stars) ataungana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala Katibu Mkuu wa TFF na  Angetile Osiah.
Wengine ni  Memeya wa Majiji na Miji ya Dar es Salaam Jerry Slaa, Gaudensi Lyimo wa Arusha, Kapinga wa Mbeya, Omari Nondo wa Morogoro, Moshi na Bukoba.

Fainali hiyo itafanyika Agosti 10 mwaka huu ambapo bingwa atajinyakulia pikipiki ya magurudumu matatu (Bajaj) na shilingi milioni moja, kombe kubwa na dogo na medali za dhahabu wa pili ataibuka na kitita cha shilingi 1.5 milioni, kombe na medali ya fedha.

June 28, 2013

GOLIKIPA DIDA WA ZAMANI WA SIMBA AJIUNGA NA YANGA MKATABA WA MIAKA 2

Hi | 11:09:00 PM | | | Be first to comment
Aliyekuwa golikipa wa timu ya Simba, Azam na Mtibwa Deogratius Munishi maarufu kama Dida amejiunga rasmi na klabu bingwa ya Tanzania bara - Dar Young African.

May 16, 2013

MARTIN SAANYA REFA ATAKAYECHEZESHA PAMBANO LA SIMBA NA YANGA SC LA KUFUNGA PAZIA LA LIGI KUU YA VODACOM

Hi | 7:34:00 PM | | | | Be first to comment
REFA Martin Saanya kutoka Morogoro ndiye atakayechezesha pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga SC la kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mchezo huo, unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini ili kujionea nani zaidi baina ya miamba hiyo, Saanya atasaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha na Jesse Erasmo kutoka Morogoro, wakati refa akiba atakuwa ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamisaa wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi atakuwa ni Leslie Liunda wa Dar es Salaam.

March 20, 2013

January 18, 2013

RATIBA YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA - 2013

Hi | 2:13:00 PM | | Be first to comment
Ratiba nzima ya mashindano ya kombe la mataifa ya Africa yatakayofanyika kule Afrika ya kusini kuanzia jumamosi ya wiki hii yani tarehe 19, 2013 ambapo mechi ya kwanza itakuwa ni Afrika ya kusini na Cape Verde.

January 17, 2013

October 22, 2012

Wateja wa Barclays kushuhudia Ligi Kuu ya England (BPL) live

Hi | 6:46:00 PM | | Be first to comment
 Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Towo Kavishe (kushoto) akionyesha jezi halisi ya timu ya Arsenal ikiwa ni moja ya zawadi watakazopewa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo. Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia tiketi ya yeye na mwenzake kwenda kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo nchini Uingereza. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Maggid Bakari na Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa benki hiyo, Samwel Mkuyu.
Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Rukia Kizwi (kushoto) akitoa tiketi ili kumpata mmoja wa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo. Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia tiketi ya yeye na mwenzake kwenda kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo nchini Uingereza na wengine wawili hujishindia zawadi ndogondogo. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa Barclays, Tunu Towo Kavishe, Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa benki hiyo, Samwel Mkuyu, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid na Ofisa Mawasiliano wa Barlclays, Lilian Machare.

October 18, 2012

NCHI TISA KUSHIRIKI ROCK CITY MARATHON 2012 OKTOBA 28

Hi | 4:26:00 PM | | | Be first to comment

 
 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania, Dioniz Malinzi (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa wadhamini wa mbio za Rock City Marathon 2012, wakifuatilia uzinduzi wa maandalizi ya mbio hizo uliofanyika kwenye Hoteli ya New Afrika. Rock City Marathon zitafanyika Oktoba 28 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Oktoba 28.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 5, Meneja Matukio wa Kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu Rock City Marathon 2012, Grace Sanga jijini Dar es Salaam hivi karibuni kama sehemu udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Oktoba 28 Oktoba. Airtel pia walikabidhi fulana 400 zitakazotumika katika mbio hizo.
Mkali wa Bongo Flava Juma Kassim 'Sir Nature' (katikati) akiimba na Baby adaha kutambulisha shoo yao kali itakayofanyika sambamba na mbio za Rock City Marathon 2012. Kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo, Grace Sanga, wa Kampuni ya Capital Plus inayoandaa mashindano hayo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
 
JUMLA ya nchi tisa zinatarajiwa kushiriki katika mbio za kilomita 21 za Rock City Marathon 2012, zilizoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI), zitakazofanyika Jumamosi Oktoba 28 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo Grace Sanga wa CPI, alizitaja nchi hizo kuwa Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC), Australia, India, Canada na Marekani, huku akidokeza maandalizi mazuri yamechangia ongezeo la washiriki.
“Tumetuma mialiko ya kushiriki kwa wadau wote wa riadha wa nchi jirani ili wapate kushiriki Rock City Marathon 2012, ndio maana tunategemea kupata washiriki wengi zaidi kutoka nje ya nchi, kulinganisha na mwaka uliopita na maboresho ya mbio hizi yatachangia kuongeza ushindani,” alisema Grace.
Sanga aliongeza kuwa, mbio hizo za kila mwaka zimegawanywa katika makundi matano ya mbio za kilomita 21 kwa wanawake na wanaume, kilomita tano kwa watu wote, kilomita tatu kwa walemavu, kilomita tatu kwa wazee kuanzia miaka 55 na kilomita mbili kwa watoto wa kati ya miaka saba hadi kumi.
Rock City Marathon zilianzishwa mwaka 2009, ambapo mwaka huu ziko chini ya udhamini wa NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), PPF, African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mbio hizo zinazosubiriwa kwa hamu na wakazi wa Kanda ya Ziwa, zitapambwa na burudani ya aina yake kutoka kwa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Juma Kassim ‘Sir Nature’, ambapo zitaanzia kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kupitia njia tofauti na kurudi uwanjani hapo.
Aidha, Sanga alisema kuwa, pesa itakayopatikana kutokana na ada ya usajili wa washiriki unaofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, Ofisi za Capital Plus zilizopo jengo la ATC ghorofa ya tatu na kwenye blog ya rockcitymarathon.blogspot.com zitapelekwa katika mfuko wa msaada kwa watu wenye ulemavu waishio jijini Mwanza.

September 2, 2012

SERENA APAA, VENUS WILLIAMS AKIAGA US OPEN 2012

Hi | 3:07:00 PM | | | Be first to comment
NEW YORK, Marekani

Wakati Serena akisonga mbele, ndugu yake na bingwa wa zamani wa US Open, Venus Williams alijikuta akitolewa mashindanoni kwa kukubali kichapo cha 6-2 5-7 7-5 kutoka kwa Angelique Kerber

NYOTA anayeshika nafasi ya nne katika viwango vya ubora wa tenisi duniani, Serena Williams hakupata shida kufuzu raundi ya tatu ya micuano ya Wazi ya Marekani ‘US Open’ baada ya kupata ushindi wa moja kwa moja dhidi ya Mhispania Maria Jose Martinez Sanchez.

Bingwa huyo wa michuano ya Wimbledon na Olimpiki, alitumia muda wa saa moja na dakika 22 (1:22) kuibuka kidedea kwa seti mbili kwa bila za 6-2 6-4 dhidi ya nyota asiyekuwa na kiwango Sanchez.

Wakati nyota huyo akisonga mbele, ndugu yake na bingwa wa zamani wa US Open, Venus Williams alijikuta akitolewa mashindanoni kwa kukubali kichapo cha 6-2 5-7 7-5 kutoka kwa Angelique Kerber.

Nyota namba mbili kwa ubora duniani, Agnieszka Radwanska alilazimika kufanya kazi ya ziada kutoka nyuma na hatimaye kumshinda Mhispania Carla Suarez Navarro kwa 4-6 6-3 6-0.

Kwa upande wake mkali wa mchezo huo raia wa Serbia, Ana Ivanovic aliibuka kidedea na kutinga raundi ya tatu ya michuano hiyo kwa ushindi wa 6-2 6-2 dhidi ya Msweden Sofia Arvidsson.

Katika raundi ya tatu, Ivanovic anatarajia kupata upinmzani mkali kutoka kwa yoso wa miaka 19 Sloane Stephens, yoso aliyeingia katika 50 bora ya wacheza tenisi wanamama, aliyetinga hatua hiyo kwa kumchapa Tatjana Malek wa Ujerumani kwa 5-7 6-4 6-4.

Licha ya kutupwa nje ya mashindano, bingwa mara tano wa Wimbledon Venus alisema; "Nilijihisi Marekani kwa mara ya kwanza " kutokana na aina ya sapoti aliyooneshwa na kutoka kwa mashabiki wa nyumbani kwenye Uwanja wa Arthur Ashe.

"Hii ni mara ya kwanmza ambayo nimecheza hapa na kuona kundi kubwa la mashabiki likiwa nyuma yangu kama hivi. Nilisubiri uungwaji huu kwa muda mrefu, hatimaye nimeupata ingawa matokeo hayakuwa mazuri," alisema Venus.

"Ilikuwa ya kushangaza sana. Nilijisikia kama niliyeshinda dhahabu. Kiukweli ilimaanisha kitu. Kwa sasa naangalia mbele kuona namna navyoweza kutumia ipasavyo sapoti mara mbili yah ii niktakayopata katika michuano ya mwaka ujao nikiwa bora zaidi."

August 30, 2012

MTOTO KUWAKILISHA TANZANIA KUPITIA MCHEZO WA ‘TAEKWANDO

Hi | 5:16:00 PM | | Be first to comment
Jina: AikaRose Mwasha
Jinsia: Kike
Miaka: 12
Utaifa: TANZANIA
Mchezo: Taekwando
KILO: 28 kg- beginners FEMALE
Club: Nong Jang
Makazi: Leuven Belgium
MAFANIKIO: Medali Ya Fedha & Dhahabu

Kijana wa kitanzania mwenye ndoto ya kuwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa hapo usoni kwa kupitia mchezo wa mbinu za kujihami wa ‘Taekwando’ ,anamapenzi makubwa na mchezo huu aliouanza angali mdogo akiwa na umri wa  miaka 9 ,ameshashiriki mashindano madogo madogo nchini Belgium na kupata mafanikio makubwa kufikia medali ya fedha. Hivi karibuni alifanikiwa kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olympic open Brussels yaliyofanyika Rue Du Lombartzyde Brussels, Belgium tarehe  27 May 2012.

August 13, 2012

JAMAICA TAKES GOLD,SILVER & BRONZE IN OLYMPICS 200M

Hi | 7:47:00 PM | | Be first to comment
Usain Bolt won the men's 200m in emphatic style tonight, earning his title as the world's greatest ever sprinter. The Jamaican powered home in 19.32 seconds, just a fraction outside the Olympic record of 19.30 - and he raised the roof on the Olympic Stadium by dropping to the track and celebrating by doing press-ups. Yohan Blake and Warren Weir made it a Jamaica one-two-three.

August 9, 2012

OKWI MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA SIMBA, APEWA TUZO YAKE ASHANGILIA NA MASHABIKI

Hi | 5:33:00 PM | | Be first to comment
Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi akionyesha tuzo yake aliyozawadiawa na klabu ya Simba baada ya kuwa mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo kwenye tamasha la siku ya simba linalofanyika kila mwaka.
Mashabiki nao walinogesha kwa kumuongezea zwadi ya jezi iliyopewa jina la Okwi Hakunaga.

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster