Mfumo
endeshi wa Android katika vifaa vya mawasiliano hasa simu ni miongoni
mwa mifumo inayoonekana kufanya vyema na kutumiwa sana duniani kwa sasa.
Android ulioanzishwa ulivumbuliwa na Andy Rubin, Rich Miner, Nick Sears na Chris
White huko Palo Alto, California,Marekani walianzia mbali katika maendeleo yake.
Walikuwa
wanalengo la kutengeneza programu za komputa kwa ajili ya kamera lakini
baada ya kugundua kuwa kamera hazina soko kubwa waliamua kuanzisha kwa
siri mfumo wa Android ili waweze kushindana na mifumo endeshi ya
Symbiani na windows
Agosti
17,2005 kampuni ya Google ilihitaji japo waanzilishi hawa hawakufahamu
kama kampuni hiyo ya mawasiliano ya intaneti itaweza kuingia katika soko
la simu za mikononi kwa hapa ilipofikia.
Toka
mwaka 2008, Android imekuwa ikitoa na kufahamika kwa matoleo yake
ambayo ni Alpha 1.0, Beta 1.1, Cupcake 1.5, Donut 1.6, Éclair 2.0 – 2.1,
Froyo
2.2 – 2.2.3, Gingerbread 2.3 – 2.3.7, Honeycomb 3.0 – 3.2.6, Ice Cream
Sandwich 4.0 – 4.3.1, Jelly Bean 4.1 – 4.3.1, Kitkat 4.4 – 4.4.4 na
Lollipop 5.0 – 5.0.2

0 COMMENTS:
Post a Comment