Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitangaza kujiuzulu
mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
TAARIFA Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameamua kujiuzulu nafasi yake. Profesa Muhongo ametangaza hatua hiyo leo asubuni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
akitangaza kujiunzulu mbele ya waandishi wa habari mapema leo
Jumamosi Januari 24, 2015 makao makuu ya wizara ya Nishati na Madini,
jijini Dar es Salaam Waziri wa nishati na Madini, Profesa sospeter
Muhongo, ametangaza kujiuzulu kutoka wadhifa huo mapema leo Jumamosi
Januari 24, 2015.
Waziri huyo mtaalamu wa miamba, amejiuzulu kufuatia shinikizo la muda
mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya
bunge lililopita, lililoiagiza Serikali kuchukua hatua dhidi ya viongozi
wote na watendaji waliohusika na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow
iliyobainisha kiasi cha fedha bilioni 302 kuchotwa BOT zilipokuwa
zikihifadhiwa.
Mwishoni mwa mwaka jana, 2014, Bunge la Tanzania lilitoka na maazimio
ya kutaka kuwajibishwa kwa mawaziri Profesa Sospeter Muhongo, Profesa
Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema,
kutokana na sakata la uchotaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow,
iliyokuwa Benki Kuu (BoT) kwa kutaka mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi
wao. Mbali na hao, yumo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Eliakim Maswi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco).
Profesa Muhongo anakuwa ni kigogo wa nne kufuata mkumbo baada ya
Waziri Profesa Anna Tibaijuka kufukuzwa nafasi yake na Rais, Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema kujiuzulu mwenyewe, huku Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akisimamishwa na Bodi
ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunjwa.
Katika hotuba ya mwisho ya Rais Jakaya Kikwete, siku alipotengua
uwaziri wa Profesa Anna Tibaijuka alisema amemeweka kiporo Profesa
sospeter Muhongo wakati uchunguzi zaidi wa kashfa hiyo ukifanywa.
Taarifa zaidi ni hapo baadaye.
Taarifa zaidi ni hapo baadaye.

0 COMMENTS:
Post a Comment