Kazi kubwa ya mwongozaji ni kuhakikisha
anatengeneza filamu nzuri na yenye ubora wa kimataifa, akitumia vema
vipaji vya waigizaji anaofanya nao kazi. Waongozaji wengi hasa wale wa
Hollywood, bollywood walianza safari yao ya kuwa waongozaji kwa kuanza kuigiza, lengo lao likiwa ni kuijua vizuri tasnia ya uigizaji.
Ujuzi wa kuigiza unaweza kuwasaidia wale wote wanaopenda kuwa waongozaji wa filamu kujifunza mbinu na mitindo mbalimbali inayotumiwa na waongozaji mbali mbali kuongoza filamu, ni dhahiri kuwa kila mwongozaji wa filamu ana staili na mtindo wake wa kuongoza filamu.

Waongozaji wengi wazuri ni wale ambao historia yao pia ilianzia/ inaanzia kwenye uandishi wa muswada (script), mwandishi wa filamu ndie anayetengeneza taswira na mwongozo wa namna filamu itakavyokuwa, akipakingilia vizuri wahusika, maneno na matukio katika uandishi wake.
Tafiti zinaonyesha kwamba karibia waongozaji wote maarufu na bora wa filamu duniani ama kutoka Hollywood au Bollywood walishaandika/ wameandika miswada ya filamu mbalimbali kabla ya kuwa waongozaji, kwa mfano mwongozaji wa Hollywood Mery Gibson licha ya kuwa mwongozaji, ndiye aliiandika muswada wa filamu maarufu ya “Apocalypto” ya mwaka 2006.
KUINGIA KATIKA TASNIA YA FILAMU
Ni dhahiri kwamba wale wote wanaotaka kuwa waongozaji wazuri wa filamu ni lazima wawe na malengo, moyo wa kujituma, ubunifu, uvumilivu, waweze kupokea changamoto kutoka kwa wadau mbalimbali wa filamu na kuzifanyia kazi ili waweze kufanikiwa na kufanya vizuri katika tasnia hii pana na yenye ushindani na changamoto nyingi.
Kabla hata ya kwenda kwenye shule ama vyuo vinavyofundisha mambo ya filamu na uongozaji wa filamu ni muhimu mtu akaanza kwa kujifunza yeye mwenyewe kwa kuangalia filamu/ sinema nyumbani ama kwenye majumba ya sinema, na sinema zinazoangaliwa lazima ziwe na ubora, isiwe mradi simema/filamu.
kusoma vitabu vinavyoelezea historia ya filamu, kufuatilia mitandao mbalimbali inayoandika habari kuhusu mambo ya filamu na kuhudhuria matamasha mbali mbali ya filamu yanayoandaliwa kama tamasha la kimataifa la filamu Zanzibar (ZIFF), European film Festival “EFF” na mengine mengi lengo hasa likiwa ni kujifunza mbinu mbalimbali ambazo waongozaji wa ndani na wa nje ya nchi wanatumia kuongoza filamu.

0 COMMENTS:
Post a Comment