
Hakuna jibu la moja kwa moja ambalo linaelezea mtu anawezaje kuwa mwongozaji wa filamu.
Swali la msingi la kujiuliza ni kwamba:
Mwongozaji “ Director” hasa ni nani katika tasnia ya filamu/sinema?
jibu lake laweza kuwa ni fupi, ni mtu anayetengeneza taswira ya namna ya kuwasilisha muswada (script) kuwa maisha halisi, anachagua na anawaongoza wahusika kuweza kuwasilisha ujumbe kama ulivyokusudiwa,
Watu wengi wamekuwa wakitamani au kuwa na Ndoto za kuwa waongozaji wenye mafanikio na maarufu kama James Cameroon, Michael Moore, Mery Gibson, Tsai Ming – Ling, Ang Lee, George Lucas, Tim Burton na wengine wengi.
Lakini mafanikio hayo mtu anaweza kuyapata kwa namna gani?.
Mtu anawezaje kuwa mwongozaji wa filamu?
Hakuna jibu lolote la kujitosheleza ambalo lipo na linaelezea ni kwa namna gani mtu anaweza kuwa mwongozaji wa filamu. Ingawa unaweza Kusema kuwa mtu anaweza kuwa mwongozaji wa filamu kwa kuchukua video kamera na kuanza kuongoza.
Swali la msingi hapa ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuwa mwongozaji mweledi?
0 COMMENTS:
Post a Comment