USHUHUDA WA KUTISHA “NIMEAMBUKIZA MAELFU YA WATU VVU KATIKA JIJI LA DAR”
Mimi
ni Jane naishi mwenge Dar es salaam naomba utalifuta jina la baba yangu
maana sitaki liwe kwenye blog watu watanijua na kuniangamiza maana
nimeshawaangamiza wengi sana kwa UKIMWI ila mengine yote usifute hata
moja ili dunia ijue tu japokua mimi nitakufa kwa huu ukimwi nilionao.
Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na hata
sikujihusisha na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya
kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa Mwenge.
Nilipata marafiki wengi tu na kuna kijana mmoja alinitongoza kwa muda
mrefu sana na siunajua vijana wengi hutumia muda mrefu kutongoza ili
msichana unadhani kwamba labda huyo anakupenda kumbe anataka tu ngono na
wadada wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda mrefu na mvulana basi
huyo yuko serious kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia tukawa
wapenzi ila nilikataa kuhusu kufanya mapenzi maana anayekupenda kiukweli
sio uongo lazima asitake ngono kabla ya ndoa.
Kwa miezi kama 5
hadi 6 aliniambia kuhusu kufanya mapenzi nilikataa alitumia mbinu
nyingi sana kwa kunibembeleza na hata kulia mbele yangu ili tufanye tu
mara moja ila nilikataa, alisema atavumilia hadi siku ya ndoa yetu
ambapo tulipanga kuoana mwaka sept 2009.
Siku moja aliniambia
twende kwenye kumbi za starehe na mimi kwa sababu ya upagani na
kumwamini pia kwa sababu nampenda nilikubali tulienda huko na kulikua na
bendi fulani maarufu ya mziki wa dansi ilikua inatumbuiza.
Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi wangu akaagiza pombe alianza kunywa
huku akinionjesha, nilikataa kwa sababu nilikua sijawahi kunywa pombe
katika maisha yangu yote, hata sijui alinishawishi vipi nilijikuta
nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa tulikaa pale kwa muda zaidi ya masaa 5
nadhani nikunywa kama bia 3 au 4 japokua nilikua nakunywa kidogo kidogo
tu tena kwa kunywesha na mpenzi wangu maana nikama nikua nanyweshwa
kila baada kama ya dakika 25 ndipo nakunywa mara moja na sikujuia kama
nakunywa pombe ila niliihisi tu naonja ili kumlizisha mpenzi wangu.
Ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi usingizi na pia nilijiona wa tofauti
najua nililewa hata kama sikujua kama nimelewa maana nakumbuka tulitoka
pale huku amenishika mkono huyo mpenzi wangu. Tulikodo tax na kuondoka
na siku hiyo aliniambia twende kwake alikokua amepanga chumba maana
tulikua na usingizi sana nilikubali huku nikidhani hatuwezi kufanya
mapenzi.
Tulifika salama na kuingia ndani ukweli pombe ni
kichocheo cha ngono na ningekua mimi ndio Raisi wa Tanzania ningefunga
bar zote. Nilijikuta natamani kufanya mapenzi na huyu mpenzi wangu hata
alikua hana nia maana alijua atanichukiza sana na uhusiano ungekufa siku
hiyo lakini kwa sababu ya pombe nilimwambia siku hiyo tufanye kidogo
maana mwili wangu unataka.
Ni kweli siku hiyo kwa sababu ya
pombe nilifanya mapenzi na huyo mpenzi wangu na baadae akanipeleka
nyumbani baada ya wiki mbili maana tulikaa wiki mbili bila kuonana
alikuja na kunieleza habari ambayo sikuihitaji katika maisha yangu maana
nilikua nasikia tu kwa watu wengine lakini sio kwangu alisema ”JANE
ISHI KWA MATUMAINI KUANZIA SASA”
Nilidhani utani lakini aliniambia kuwa yeye ana UKIMWI tangu miaka mitano iliyopita na anapenda tu ngono maana hawezi kuacha.
Nililia sana na baada ya wiki moja baadae nikaenda kupima na kukutwa
nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na chanzo cha yote ni pombe,
kupenda starehe,disko na upagani unaotusumbua wanadamu wengi.
Nilikua na UKIMWI na kwa hasira maana mpenzi wangu alihamia Arusha huku
akisema neno moja la mwisho kwamba ”shetani amemtuma kuwaambukiza
wanadamu UKIMWI”
Sikujua, sikujua, sikujua, sikujuaaaaaaaaa,
basi tu ooh YESU nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa mzigo ambao
haukunistahili mimi. Hata leo hua najiuliza kwamba nilijitunza kwa miaka
23 yote lakini pombe na huyu wakala wa shetani wamenifanyia hivi. Baada
ya kujua nina UKIMWI na hali hiyo nikaikubali na kulikua na kundi kubwa
sana la wanaume ambao walikua wamewahi kunitongoja na niliwakataa sana
kwa sababu hii niliwakubali ili nami nife na wengi.
Nilianza
kumkubali kila mmoja na kuna baba mmoja ambaye ana wake 3 niliwahi
kumtukana sana kipindi cha nyuma kila aliponitongoza lakini wakati huu
nilimkubali na hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga na
akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua kuwa
namwambukiza na hata leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao wana
UKIMWI uliotoka kwangu.
Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012
nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana ilifika kipindi nala na
wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe kama mimi nilivyokomeshwa
na nina uhakika kutokana na mimi wameambukizwa UKIMWI wanadamu zaidi ya
10,000 na hili tangazo la ”TUKO WANGAPI” huwa linaniliza kila siku maana
hata mimi najua kabisa nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa idadi
kubwa sana ya watu.
Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku
naombewa nilikutwa na mapepo mengi sana na hata waombeaji wakashangaa.
Ningejua ningeokoka tangu nikiwa na miaka 5 lakini ndio hivyo sina jinsi
wala uwezo wa kubadirisha hali hiyo.
Na naomba kila
atakayesoma ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni dhambi pia kwenda
disko ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi na kila kichochoe chochote cha
dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi kujua kama nina UKIMWI na
sijui MUNGU ana mpango gani na mimi maana kwake yote yanawezekana.
Nauamini uponyaji wake na sijawahi kutumia ARV hata siku moja na afya
yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe kujua kama uovu huu nimefanya
mimi.
Ndugu zangu kama una UKIMWI nenda kanisani ukaombewe na
kama una akili mpe YESU maisha yako maana pia baada ya kifo ni hukumu.
Yasalimishe maisha yako kwa YESU na usiambukize wengine tena.
Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi tena na sitafanya hivyo wala
sitaolewa na mtu yeyote maana yatosha kwa uovu niliofanya na hadi sasa
wapo ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki na nilihudhulia misibani huku
nikijua kabisa chanzo ni mimi.
Mwisho nawashauli wababa
kulidhika na wake zao na wamama pia lidhikeni na waume zenu, vijana
ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa au kuolewa na kabla ya
kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye UKIMWI ni wengi kuliko
unavyozani.
Fuata unachofundishwa kanisani na pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.
MUNGU akubariki
Ni mimi Jane,
Mwenge, Dar es salaam
Tanzania
0 COMMENTS:
Post a Comment