Mkuu wa huduma za internet wa Tigo
Tanzania, David Zacharia (kulia) akiongea wakati wa uzinduzi wa
internet.org jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Naheed Hirji, Mkuu wa
ukuzaji huduma za Facebook Afrika Mashariki na Kusini. Picha na Khalfan
Said.
sehemu ya mpango mpya uliozunduliwa kati ya mtandao wa kijamii wa
Facebook kutoka Marekani na Tigo, inayotoa huduma za simu Kampuni hizo
mbili zimezindua huduma ijulikanayo kama internet.org ambayo
inawawezesha wateja wa Tigo kutumia baadhi ya tovuti bila gharama.
Internet.org
ni mpango wa kimataifa unaoyashirikisha miongoni mwa makampuni makubwa
ya teknolojia, taasisi zisizo za kibiashara zinazofanya kazi pamoja
kufikisha huduma ya internet kwa mabilioni ya watu duniani ambao
hawapati huduma ya internet.
Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Facebook yenye makao yake nchini Marekani ni waanzilishi wa internet.org.
Mkuu
wa ukuzaji wa huduma za Facebook, Afrika Mashariki na Kusini, Naheed
Hirji ameileza BBC kuwa soko la Kiswahili linakua na kwamba kampuni yake
imeona Tanzania kuna fursa ya kuwafikia watu wengi.
"Tunazindua
huduma hii Tanzania kwasababu kutokana na utafiti wetu tuliofanya, chini
ya asilimia 20 ya watu wanapata huduma ya interenet.
Kwa hiyo tumeona kuna fursa kubwa na nafasi ya kusaidia kuwaunganisha watu hawa kupata huduma za internet", alieleza Hirji.
Akafanua
kuwa: "Lugha ya Kiswahili ni muhimu sana kwetu, takriban mwaka mmoja
uliopita tulitafsiri Facebook yote ipatikane kwa lugha ya Kiswahili , si
tu kwa watumiaji wa Tanzania.
Kwa hiyo tulitafsiri Facebook yote ipatikane kwa Kiswahili ili iweze kuwawekea mazingira mazuri na kuwafikia wengi zaidi".
Taarifa
ya hivi karibuni kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania - TCRA,
ilionyesha kuwa idadi ya watu wanaotumia internet iliongezeka kutoka
milioni saba na nusu mwaka 2012 mpaka kufikia milioni tisa nukta tatu
mwaka huu 2014.
Katika uzinduzi kuna tovuti zisizopungua 15 za
makampuni ya ndani na nje ya Tanzania ambazo huduma zao zitakuwa
zikipatikana bure kwa wateja wa Tigo, ikiwemo BBC kwa lugha ya
Kiingereza na Kiswahili, vile vile tovuti ya Mwananchi.
Kampuni ya Tigo imesema inakusudia kufanya huduma kuwa endelevu na kuongeza nyingine kadri muda unavyosonga mbele.
Hata
hivyo wachambuzi wa maswala ya teknolojia wanasema lengo la kuchochea
na kuwafikishia watu wengi zaidi huduma ya internet bado litakutana na
ugumu mwingine hasa kutokana na gharama za kununulia simu zenye uwezo wa
kutumia internet kuwa kubwa na upatinaji wa umeme wa uhakika katika
baadhi ya maeneo ya vijijini, japokuwa umeme wa jua umeanza kutumika kwa
wingi.

0 COMMENTS:
Post a Comment