April 18, 2013

MATUSI YA WABUNGE AMBAYO SPIKA AMEAHIDI KUWASHITAKI POLISI

Hi | 12:07:00 AM | | | |
JOSEPH MBILINYI:
"Mambo mengi  ya  nchi  hii  hayaendi  kutokana  na  SERIKALI  PUMBAVU....
Hatuwezi  kuwa  na  WAZIRI WA ELIMU BOYA  mwenye  elimu  ya  kuunga  unga  halafu  tufanye  vizuri  katika  sekta  ya  elimu , haiwezekani."
 
LIVINGSTONE  LUSINDE:
"Siwezi  kuikubali  taarifa  hiyo.Nadhani  huyu  mtu  bado  amechanganyikiwa  na  uchaguzi  wa  kenya.Mimi  sijaitaja  Chadema bali  nimesema  kuna  chama  kimoja  cha siasa,SIJUI YEYE  ANAWASHWA  NINI..!!
JUMA NKAMIA:
Sugu  naomba  unyamaze.Mimi  ndiye  nazungumza.Mimi  siongei  na  mbwa,naongea  na  mwenye  mbwa.

Khatibu Saidi Haji (Konde - CUF)
Alimtukana Freeman Mbowe mbunge wa Hai kwa kusema "Mbowe kaja hapa anajambajamba tu" akilalamikia hoja ya Mbowe kuhusu idadi ya watu wa visiwani.

Alimtukana Mchungaji Msigwa: "Wewe Msigwa ni mchungaji wa watu au mchungaji wa nguruwe? "Alitoa tusi hilo kutokana na Mchungaji Msigwa kutoa kauli ya kwamba Zanzibar kuna udini.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster