August 19, 2012

MZEE WA MIAKA 64 AMLAWITI MTOTO WA MIAKA 4

Hi | 3:25:00 PM |
RPC SHINYANGA BW.EVARIST MANGALA

JESHI la Polisi Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Shunu, Kata ya Nyahanga, Bw. Manyanda Katulie (62), kwa kosa la kumlawiti mbaka mtoto wa miaka minne.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Everist Mangalla, ilisema Bw. Katulie anadaiwa kufanya kosa hilo juzi jioni katika kijiji hicho baada ya kumrubuni mtoto huyo na kumlawiti.

“Watu walisikia mtoto huyu alikilia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata na kwenda kumpa msaada,” alisema.

Kamanda Mangalla alisema, Bw. Katulie alimrubuni mtoto huyo wakati akitoka kucheza na wenzake na kuongeza kuwa, uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster