November 9, 2011

BALOZI WA UMOJA WA ULAYA HAPA TANZANIA AAGANA NA SPIKA ANNE MAKINDA NA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE

Hi | 11:30:00 PM |

 Spika wa Bunge Anne Makinda akimpa Balozi Clarke zawadi ya saa ya ukutani yenye jengo la Bunge la Tanzania.
 Spika Anne  Makinda akiwa na mazungumzo Balozi Clarke ofisini kwake leo
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo Pinda(kushoto)  na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (katikati) wakisalimiana na kubadilishana mawazo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa Tanzania Mhe. Tim Clarke mjini Dodoma leo. Mhe. Tim Clarke amekuja Dodoma kuliaga Bunge baada ya kuwa hapa nchini kwa miaka minne.

Balozi Clarke(kulia) pia alikutana na kujadili masuala kadhaa na  Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (katikati). Kushoto ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Khalifa Khalifa. 
Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Mussa Zungu Azzan, Bolozi wa Umoja wa Ulaya Tim Clarke, Mwenyekiti wa Kamati Mhe Edward Lowassa na Mjumbe wa Kamati  Mhe. Khalifa S. Khalifa.Picha na Prosper Minja -Bunge

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster