Rapa wa Kimarekani The Game akiwa katika Pozi
Msanii The Game jina kamili Jayceon Terrell Taylor aliyezaliwa mnamo tarehe 29 Novemba 1979 rapa wa Kimarekani na mwigizaji na akiwa mwanzilishi au mwanachama wa kundi maarufu nchini Marekani G - Unit, Mwaka 2005 alijipatia umaarufu na mafanikio makubwa ya albamu yake ya kwanza iliyotambulika kwa jina la Documentary, ambayo ilimwezesha kupata Tuzo mbili za Grammy Award nominations. Ikifuatiwa na album nyingine iliyokwenda kwa jina la Doctor Advocate miaka ya 2006, na albamu yake ya tatu iliyotambulika kama Lax mwaka 2008. Na pia ana studio ya kurekodi ijulikanayo kama Black Wall Street Records.
Msanii huyu siku ya jumanne ya tarehe 23 mwezi 8 mwaka 2011 alisikika katika vyombo vya habari akinena kuwa mwisho wa Dunia umefika ikiwa ni mwaka 2012, na maamuzi aliyochukua ikiwa ni hatua ya maandalizi ya mwisho wa dunia ameweza kuviambia vyombo vya habari kuwa kuanzia mwezi huu anaandaa maghala ya vyakula vya kila aina katika nyumba yake ili kuinusuru familia yake na njaa, Pia alisikika akisema hatatoka nyumbani kwake kwa kuanzia mwezi wa 12 na atakuwa analea familia yake kwa jumla, Pia kwa kuongeza alisema kuna viumbe vya ajabu na hatari ambavyo vitakuja kuingamiza Dunia. Alimaliza kwa kusema anaomba mjihadhari na kufuata nyayo zake akiwa kama mtabiri.
Pia katika Historia ya haya maneno ya msanii huyu kipindi cha nyuma kuna mtumishi wa Mungu Nchini Marekani aliwahi kutairi usemi kama huu lakini haukuzaa matunda, Je msanii huyu tunapaswa kumwamini kwa maneno aliyotamka? Swali kwako Mtanzania..!
1 COMMENTS:
alikuwa amekula bange siku hiyo
Post a Comment