July 6, 2011

Wamachinga wapambana na Polisi Jijini Mwanza

Hi | 1:14:00 PM |
Mapambano dhidi ya machinga na polisi jijini Mwanza yanazidi kupamba moto! Na kifupi hali si shwari kabisa kwa siku ya leo, Fujo bado zinazidi kupamba moto chanzo chake bado hakijapatikana. Hadi sasa kuna tetesi kuwa vijana wawili wamekufa  wakati polisi walipokuwa wakikabiliana na machinga hao.Tanzania ni nchi ya Aman??!!! Viongozi  mnahitaji kuweka mikakati iliyothabiti kuinusuru Taifa. Vijana wanakadiriwa kuwa nusu ya idadi ya watu Tanzania, na ndiyo productive age ambayo kama wataendelea kutothaminiwa Taifa litaendelea kuteketea.
 Tazama clip fupi kutoka eneo la tukio sehemu iitwayo Rwagasole Jijini Mwanza
 Watu wanakimbizana ili kuokoa nafsi zao.
Mpaka natoka eneo latukio hali haikuwa salama kabisa Blog hii itaendelea kukupasha  habari ya matukio  kadri muda unavyokwenda

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster