July 6, 2011

Lori la mkaa lapinduka LIVE..!!

Hi | 6:42:00 PM |
Nikiwa katika harakati za kuwahi kazini majira ya saa 7.45 eneo la Thaqafa Secondary school mbele kidogo, Nilikuta Gari aina ya Lori limeanguka kama limelazwa chini, Katika hali isiyo ya kawaida katika kudodosa habari nilikutana na kijana mmoja na kuninyetisha ndogo ndogo kuwa hakuna mtu yeyote aliyepata kilema wala kupoteza maisha, Kijana huyo alinipa taarifa kuwa hakujua chanzo cha ajali hiyo, Sali kabla hujasaliwa kwani hujui siku ya kufa ikiwa ni saa, dakika, na sekunde pia.
Hii ndio hali halisi kutoka eneo la tukio kwa kweli ilikuwa ni kitu cha kushangaza sana.
Kila aliyepita eneo hilo alibaki mdomo wazi kwa mashaka na kutaka kujua kulikoni, kifupi Mungu alinusuru roho za watu kwani hakuna aliyepata hata kovu sehemu ya mwili.
Karibuni kwa mara nyingine kwa habari na matukio na
www.ramsoict.blogspot.com

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster