Nimepata wasaa mfupi wa kuweza kuwaonyesheeni matukio yalotokea siku ya jana kati ya Machinga na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza, Kwani hali ya hewa ya Mji ilikuwa imegeuka kama Iraq kwani kila mtu alikuwa akikimbia kunusuru roho, na wengine walionekana kuwa na roho ngumu zaidi ya mnyama simba wakidai Haki kwa kuteketeza baadhi ya mali za watu wasio kuwa na Hatia Yeyote...!! Ungana nami kuangalia matukio haya japo kwa kifupi kutoka Jijini Mwanza.
Angalia clip hizi zilizoonyesha hali halisi ya Mji wa Mwanza kwa siku ya jana.
Hali haikuwa shwari kabisa kama unavyoona pichani Gari ya Mukesh ikiwa
imepasuliwa vioo.
Gari ambalo sikulitambua hata ni aina gani likiwa limechomwa na wananchi wenye hasira kali.
Hali haikuwa salama hata kidogo mtu asikwambie na ilikuwa kama muda wa masaa 5
Hata watu walio kuwa katika mizunguko yao hakuwa na amani juu ya usalama wao kwani kila mtu alikaa kwa mshangao na macho yakiwa juu kama mkungu wa ndizi.
Jengo hili walilichakaza sana kwa kupiga mawe na kupasua vioo vyote kama unavyoona pichani.
Gari ikiwa imebaki kama skelaton ya binadamu, Hata kama ingekuwa ni wewe usingeweza kutambua kuwa ilikuwa ni gari ya aina gani.
Fanya fujo uone kwa maana ya FFU walikuwepo eneo la tukio kwa ajili ya usalama wa raia na mali zao ila haikuwa kazi rahisi kama unavyofikiri kwani wamachinga wenyewe ilibidi wachukue nafasi ya kutuliza ghasia wenyewe kwa kukamata watu walioonekana kuwa ni vibaka na wezi.
Mungu awalaze mahali pema peponi kwa wale waliokisiwa kupoteza dunia siku ya tukio hili na wale walio na majeraha awabariki wapate kupona kwa nguvu zake. Ameni
Karibu kwa mara nyingine katika blog yangu ya habari na matukio mbali mbali
www.ramsoict.blogspot.com
Mwanza-Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment