Jana kuamkia leo majira ya saa 3: 15 eneo la Nata Jijini Mwanza kuna Hotel iitwayo Coconut Hotel iliwaka Moto mkali sana na chanzo chake ikiwa ni huu umeme wetu wa majira, Hili ni ombi kwa serikali tunaomba mboreshe huduma ya umeme kwa jamii kwani kwa njia hii hali si shwari kabisa, Sisi kama wananchi tunahofia maisha yetu kwa huu umeme wa kubeep, Mpaka natoka eneo la tukio sikuwa na hakika kama kuna mtu aliyepoteza maisha, ingawa juu ya jengo hilo kulikuwa na watu zaidi ya 10 ambao walikuwa wakipiga kelele za hapa na pale kuomba msaada, Nilikaa eneo la tukio takribani nusu saa tangu Hotel hiyo ikiteketea, Gari la zima moto lilionekana likija kwa kasi ya ajabu na kufika na kuanza kuzima mioto iliyowaka kama inapulizwa na mafuta aina ya Petroli.
Hii ndio Hotel ya Coconut iliyopo eneo la Nata jijini Mwanza iliyoungua kwa Moto mkali
Hii ndio Hotel ya Coconut iliyopo eneo la Nata jijini Mwanza iliyoungua kwa Moto mkali
Zima moto likiendelea na matukio
Umeme umekuwa kero sana hasa huu wa kukatika mara kwa mara na ndio uliosababisha hali hii.
0 COMMENTS:
Post a Comment