July 13, 2011

Nusura kukatwa mkono wooote kwa panga Tarime

Hi | 1:30:00 PM |
Ukatili tunaaamini upo katika kila nchini ingawa katika tathimini fupi kuna baadhi ya nchi hali si ya kawaida kabisa na inatishia Amani, Furaha, Upendo, uhuru wa nafsi na mengineyo katika jamii zinazotuzunguka,
Tazama hali hii ilivyomkuta dada huyu mwenyeji wa eneo la musoma ambapo ukatili kwao wanaamini ni kitu cha kawaida kabisa, Dada huyu alikatwa na Kisu aina ya Sime kama wanavyoiita wenyeji wa Mkoa Huo,
Kisa mkasa cha huyu dada ni kwamba mume wake ni mlevi hiyo kila anapokuja amelewa nyumbani kwake huja kwa hasira kila siku na kuanza kutukana matusi yasiyo kuwa na idadi wakati mwingine huamua hata kutoa kipigo ingawa huwa si kawaida ya hii hali iliyotokea, siku kabla ya tukio alimuaga kuwa anaelekea kunywa pombe na akirudi asimkute, Baada ya kurudi jioni alifika na sime yake na kuanza kumkuta akianzia kichwani, mgongoni mpaka kwenye mkono, mdada huyu alianza kupiga kelele na baada ya hapo majirani ndio walionusuru roho ya huyu dada, mwanaume alikamatwa na sasa yupo lupango, ila mpaka sasa mdada huyu anaendelea vema na matibabu hali yake ni nzuri na ya kulidhisha kwa sasa.
Naomba tuamini kuwa ukatili si sehemu ya maisha yetu na tunapaswa kuupinga ikiwa wewe ni mzee, kijana, msichana, mtoto, kwani tukisema hapana kwa sauti ya pamoja naamini tunaweza kuondoa aina zozote zile za ukatili kwa jamii zetu za kiafrika,
 Dada huyu alipigwa na mume wake nusura amtoe roho kwa kufanikiwa kumkata kipande cha nyama katika mkono, amini ukatili upo na unaendelea kwa baadhi ya maeneo.
Hali hii ilimkuta mdada huyu Musoma eneo la Tarime
Tupinge ukatili kwa pamoja ili kuleta familia zilizo na kwa vizazi vyetu.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster