Kivulini imeandaa mafunzo ya jinsia na haki za binadamu kwa wasichana yaliyoanza leo tarehe 13/06/2011 yatamalizika tarehe 17/06/2011 siku ya Ijumaa. Jumla ya wasichana 37 wenye umri kati ya miaka 15 na 20 katika jij la Mwanza walioko ndani na nje ya shule watashiriki katika mafunzo hayo.
Katika mafunzo hayo ya siku tano, wasichana hao watajifunza kuhusu suala la jinsia, maana yake na pia watachambua majukumu mbalimbali ya kijinsia kati ya wanawake na wanaume ili kuweza kutambua nafasi zao katika jamii na kama wasichana na viongozi wa kike wa kesho
Katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo, washiriki wamejifunza pia kuhusiana na suala la nguvu na matumizi yake katika jamii na kama kisababishi cha ukatili dhidi ya wanawake.
Wawezeshaji katika mafunzo hayo walikuwa ni Bi Celestina Nyenga na Jovitha Mlay wote wafanyakazi wa Kivulini katika programu ya Utetezi na Sera.

Bi. Celestina Nyenga akiendesha mafunzo kwa vijana na anaongea kwa hisia mno
Kijana akiwasilisha kazi za vikundi walizopewa na wawezeshaji
Angela naye alikuwa ni mmoja wa washiriki aliyetoka Geneva juzi alikowasilisha mawazo ya watoto wafanyakazi wa Nyumbani
Mshiriki akichangia mawazo
Washirki wote
Sura zote ziko makini sana kusikiliza kinachojiri
Tunaendelea uskose kwa wakati mwingine
1 COMMENTS:
hongera sana vijana kwa kushiriki vema katika mafunzo yenu msikate tamaa bali mzidishe juhudi kuelewa kinachozungumziwa
Post a Comment