June 11, 2011

WANAFUNZI WA ST. AUGUSTINO WATUTEMBELEA KATIKA MAFUNZO YETU.

Hi | 1:20:00 AM |
Leo katika mafunzo yetu ya mbinu za uongozi kwa wasichana tulitembelewa na baadhi ya wanafunzi kutoka  katika Chuo cha Mtakatifu  Augustine Jijini Mwanza maarufu kama SAUT, waliowatembelea  washiriki  wa semina hiyo. Wageni hao ambao ni Waziri wa Jinsia na Maendeleo ya Jamii wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho na ambaye ni Mwanasheria mtarajiwa wa mwaka wa pili Bi  Juliana Ezekiel na  Makamu wa Raisi wa Serikali ya wanafunzi  Bi. Anna Mushi walielezea uzoefu wao kama viongozi wanawake chuoni hapo.
 Bi  Anna Mushi ambaye ni  makamu wa raisi wa chuo hicho anasema kuwa kwa msichana kiongozi ni lazima ajiamini. Alieleza pia sifa za kiongozi bora kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kutatua matatizo, , mwenye uwezo wa kuzalisha, kuchuja mambo na kutoa yaliyo bora na yenye manufaa, anayefanya kazi kwa manufaa ya wengine na sio kwa manufaa yake mwenyewe na anayebadilika kutokana na maoni ya watu. Aliongeza pia kuwa kiongozi ni kioo cha jamii. Aliongeza pia kuwa vitu vya msingi kama kiongozi bora ni lazima amche Mungu, ajitume, ajitambue yeye ni nani, anatakiwa kufanya nini, wakati gani, wapi na kwa nini na awe na malengo na ndoto.  Kwa kauli hiyo, washiriki wa semina hiyo walijiuliza kama viongozi walioko madarakani wanafuata misingi hiyo.
 Bi. Anna akiongea kwa hisia kwa vijana katika mafunzo
 VIONGOZI NA MAVAZI
Makamu wa raisi alieleza pia kuwa mwonekano wa nje wa kiongozi mwanamke ni jambo la msingi sana.  Ili kuonekana kuwa ni kiongozi unayefaa, ni lazima avae mavazi yenye heshima na yatakayomsitiri vizuri mbele ya watu. Anasema kuwa mavazi ni kielelezo cha tabia ya ndani ya mtu.
Bi Anna alieleza kwamba, kwa kutambua hilo, Uongozi wa Chuo cha Mt Augustino umepiga marufuku uvaaji wa suruali na mavazi ya kubana kwa wasichana chuoni hapo. Amri hiyo imetokana na marekebisho ya sheria ndogo za chuo hicho yaliyofanyika katika juma hili. 
 Bi. Anna akiwa anasikiliza vijana kwa makini na akitabasamu
  Alishiriki vema mdada huyu
  Bi. Juliana ambaye ni mwanasheria kutoka chuo cha Mtakatifu St. Augustino Jijijni Mwanza akiongea na vijana kwenye semina, alifafanua na kuwaeleza kuwa unapokuwa msichana lazima utambue haki zako za msingi na kuweza kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo kwa wavulana hasa wanapokuwa wakidanganyika na kuahidiwa kuolewa na wajue kuwa wanapokuwa wanafuata na vijana na kupewa ahadi zisizo za ukweli. Alieleza kuwa pia ili kuwa mtu unayetaka kufanikiwa maishani lazima uwe na malengo na ndoto, kuwa na mipango na namna ya kutekeleza mipango hiyo.
  Washiriki walitamani sana jinsi wana chuo hao walivyokuwa wakizungumza kuhusu ndoto zao
 Mshirki aliyekili kubadili mavazi yake hasa suruali alisema hata vaa tena kwani mabinti hao kutoka chuo cha mtakatifu St. Augustino walimjengea uwezo wa kubadili mwenendo wa Tabia na mavazi.
 Baada ya hapo tulipga picha ya pamoja kama ukumbusho wa siku ambayo hatuna hakika kama tungeweza kukutana tena kwa mapenzi ya Mungu.
 Walipendeza kila mmoja washiriki
 wote walijawa na tabasamu ambalo sikuwahi kuliona hata wakati napiga picha hii nami nilikuwa nafurahia sana kiasi kwamba mpaka nilishindwa kujizuia kwa kicheko cha furaha
 Bi Jovitha Mlay alipendeza sana na wigi lake alilonunua nchini South Africa
  Mjasiliamali alikaa kwa pozi jamani katikati
 Aliyechuchumaa ni Mr Benard Makachia mwenesha semina hii
Asanteni kwa ushirikiano wenu kutazama habari hii na pia shukrani za pekee toka kwa Bi. Anna na Bi. Juliana kwa kutuwezesha kushawishi vijana ambao ni Taifa la Kesho.
 Huu ndio mwisho wa semina yetu nawatakieni matajaribio mema katika shughuli mbali mbali

1 COMMENTS:

Anonymous said...

nimefurahia sana kuona wanawake jinsi mnavyowapatia kipaumbele kivulini muendelee na moyo huo huo msikate tamaa

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster