June 14, 2011

Maazimisho ya siku ya mtoto wa Africa

Hi | 9:19:00 PM |
 Maazimisho ya siku ya mtoto wa Africa,
Pamoja You club ni kikundi cha jumla ya vijana 20 kinachopatikana Jijini mwanza kilichoanzishwa mnamo mwaka 2009 kupitia shirika lisilo la Kiserikali Kivulini, Vijana hao wana malengo yao mbali mbali ikiwa ni pamoja  na kuendeleza haki za watoto wote wanaonyanyasika majumbani, Siku ya leo vijana hao wameandaa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Africa ambayo yanafanyika katika Ukumbi wa Mwanza Sekondari , maada mbali mbali ziliendeshwa ikiwa ni pamoja na “Je, kuna mabadiliko yoyote juu ya ukatili dhidi ya watoto katika miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania
 Kijana mmoja Pichani aitwae Emmanuel  mwanafunzi wa Mwanza Sekondari alisema kuwa mabadiliko yapo ingawa ni kidogo ukilinganisha na hapo zamani, anapenda na amefurahishwa na maada ya leo kwani ni kweli watoto wengi wapo majumbani kwetu ambao hawapewi  haki zao za msingi kama kusoma, kupata muda wa kupumzika na mengine, hasa hii alisema hutokea kwenye familia ambazo wana kipato duni, kuwa unakuta mtoto anakatazwa na wazazi wake kwenda shule na anaambiwa aende akauze karanga kwa ajili ya kulisha familia.
 Vijana wamekaa kwa utulivu wakisikiliza maada
 Uzuri wa maazimisho yalihudhuliwa na watoto wengi ilikuwa ni safi sana kwani tulisikiza mawazo yao mengi
 Baada ya kusoma kitabu cha athari za ukatili walishangaa sana na wengine walisema hata kwao wanaona ukatili wa namna hiyo ukitokea.
 Huyu ni msanii amabye daima anapenda kuelimisha rika au vijana kwa njia ya nyimbo miondoko aina ya Hip Hop aliwakilisha vema
 Hakuwa mbali sana na steji kama unavyomwona
 Hakika siku ya leo ametufanya kujiskia burudani sana hata siamini kabisa
Vijana na pozi kama unavyowajua mm sisemi sana unajionea mwenyewe

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster