Kivulini Shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana kwa kushirikiana na shirika la Anti-Slavery na Children Unite yote ya nchini Uingereza kupitia mradi wa watoto wafanyakazi wa nyumbani, mwaka huu tulikuwa tunaandaa mapendekezo kutoka kwa wafanyakazi wa nyumbani kwa ajili ya kuyawakilisha kwenye mkutano wa kimataifa wa ILO uliofanyika huko Geneva, Switzerland ili kuwashawishi wajumbe wa ILO ili kuwa na tamko linalowalinda watoto wafanyakaziwa wa nyumbani dhidi ya ukatili, unyanyasaji na unyonyaji. Lengo la kuandaa mapendekezo hayo ni kuboreshwa kwa haki za watoto wafanyakazi wa ndani ambazo zilikuwa zinajadiliwa na baadhi ya viongozi toka umoja wa Mataifa, hivyo sisi Kivulini kama wawakilishi toka Tanzania tuliweza kuwapeleka watoto wawili Angela na Angelina, Pia waliondoka na mlezi aliyeitwa Bi. Glory Mlaki, waliohudhulia mkutano huo nchini Swiziland Geneva, wameenda na walikaa wiki mbili na leo ndio ilikuwa siku ya kuwapongeza kwa kufika salama na kutupatia dondoo toka ughaibuni karibu na endelea kuangalia mchakato mzima.
Huu ndio mwanzo wa kuwapokea toka Airpot Jijini Mwanza ilikuwa mida ya saa 3 Usiku
Wakijiandaa kupanga mizigo yao kwa ajili ya kurudi nyumbani
Baada ya kuwasili katika shirika la Kivulini lililopo Isamilo Jijini Mwanza na kutoa pongezi kwa Mkurugenzi Bi. Maimuna Ahmad Kanyama
Kulia ni Angel na kushoto ni Angela wawezasema ni mapacha kwani wamefanana sura mpaka majina, tylifanikiwa kuwafanyia taflija fuli iliyohudhuliwa na washiriki 200 sherehe hii tulifanyia katika shirika la Kivulini Isamilo Mwanza
Hawa ni baadhi ya washiriki katika hafla fupi ya leo
Huyu alikuja amekula maana yake ndiyo hii kwani anafuta menoKila siku za Jumamos na jumapili watu huja kuogelea karibuni sana Kivulini.
Hiki ni kijogoo cha kisasa kwa kutumia Blow Out
Angela akizungumza na washiriki kwa makini
Angel nae hakuwa mbali katika kuzungumza yale yalotoka moyoni mwake hakika alifurahisha watu pole kwa kukosa mwenzangu eneo la tukio hakika tulijawa na tabasamu kila alipoongea.
Karibuni katika habari na matuki Jijini.
1 COMMENTS:
Nzuri sana mwana umeweza...
Post a Comment