June 15, 2011

Ajali ya Msukuma Tololi na Corola Tax

Hi | 12:21:00 AM |
Nikiwa katika mizunguka yangu ya hapa napale, niliweza siku ya leo kukutana na zahama la mwendesha Tololi na Baba mmoja pichani niliwakuta maeneo ya Barabara ya Salma Cone wakibishana kuwa waende mahakani baada ya mwendesha Tololi kumgonga huyo baba pembeni ya gari yake aina ya Corola Tax na kupasua taa moja ya Endiketa upande wa kushoto, kwa kweli mpaka naondoka eneo la tukio hali ilikuwa si shwari na sikujua iliendelea vipi ila inasikitisha sijui hata kama alipelekwa Polisi Je atalipa nini kijana huyo, Ni heri tu ya kusamehe wakati mwingine jamani kwani hakukusudia kabisa kwa jinsi maelezo yake nilivyoyapa kwa muda mfupi
 Huyu ndiye mwenye Tax aina ya Corola aliyevalia Jinsi na shati kachomekea
 Ungekuwepo nawe ungetamani kusimama kuangalia maana sauti ya huyu Baba ilikuwa juu sana hata mm niliogopa kwani wakati napiga picha hii pia nilikuwa natetemeka meno
Hali ilikuwa si shwari kwa hawa wasukuma mikokoteni.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster