June 5, 2011

Hafla fupi ya Kumuaga Laula.

Hi | 1:35:00 PM |
Wafanyakazi wa shirika lisilo la Kiserikali la Kivulini linalotetea Kutetea Haki za Wanawake na watoto wanaonyanyasika Majumbani wakiwa katika hafla ya kumuaga mmoja kati ya wafanyakazi wa kujitolea aliyetoka Nchini Kanada Laula sherehe hii ilifanyika katika ofisi ya Kivulini Isamilo Jijini Mwanza.
Huyu ndiye Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea haki za wanawake na watoto Kivulini lililopo Jijini Mwanza anaitwa Bi Maimuna Ahmad Kanyamala.
Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Kivulini Zacharia kulwa, Hellen James na Mayige.
Hili ndilo Jengo la Kivulini linavyoonekana kwa nje Shirika lisilo la Kiserikali linalotetea haki za wanawake na watoto wanaonyanyasika majumbani Jijini Mwanza Makao yake makuu ni Isamilo karibu na shule ya Lake Primary pia jirani na Nyumba ya Asha Rose Migiro, Karibuni sana wale wote msiopata haki zenu za msingi ndani ya familia pamoja na manyanyaso mnayoyapata tutawasaidia usisite kuwasiliana nasi kwa sanduku la Posta 11348 Email: admin@kivulini.org namba ya simu  +255754-367484 Mwanza
Pia ukifanikiwa kufika katika ofisi zetu wawezapata wasaa wa kufurahisha japo macho, tuna Swimming Pool ambapo kila siku za jumamosi na jumapili watu huja na kusherehekea na familia zao na ww waweza kuwa moja ya mshiriki ukipata taarifa hii mwarifu na mwenzio tafadhali.
Huyu ndiye Afisa Utawala wa Shirika lisilo la Kiserikali Kivulini Jijini Isamilo Mwanza, ambaye hujuliakana kwa jina la Bi Martina Mashaka, fika katika ofisi zetu zungumza naye atakupatia mengi zaidi kuhusu Kivulini.
Kivulini Kitchen ni sehemu ambayo utaweza kupata kila aina ya chakula unachopenda na pia tunapokea oda mbali mbali kama una sherehe ya aina yoyote usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba +255767-722229 tutakupatia maelezo mengi kwa kina karibuni sana tupo Isamilo karibu na Shirika la Kivulini Mwanza.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster