June 17, 2011

Habari njema kwa watoto wafanyakazi wa ndani Jijini Mwanza Juu ya mafunzo mbali mbali ya kazi za mikono.

Hi | 4:15:00 PM |
Chezesha Mikono ni shirika lisilo la Kiserikali lenye makao yake makuu jijini Mwanza na lina jumla ya wafanyakazi wasiopungua watatu ikiwa ni pamoja na mwalimu wa mafunzo, linalotoa mafunzo mbali mbali ya watoto wafanyakazi wa ndani, mafunzo hayo ni kama vile, Kushona nguo, kutengeneza, Mikoba, Heleni, bangili, mafunzo ya kompyuta, Cherehani, Vikapu, kusuka mikeka, na mengine mengi zote ikiwa ni kazi za mikono kama jina la shirika lao linavyotambulika. Kuna jumla ya watoto wafanyakazi wa ndani 60 ambao huja katika mafunzo hayo kwa awamu kila jumatatu mpaka ijumaa, kuna wanaoingia  saa 2 mpaka saa 6, na wengine 7 mpaka saa 10, Na nina kadilio la jumla ya watoto 11 waliohitimu toka Shirika hilo na sasa huko waliko wanaendelea na shughuli za kujiingizia kipato ikiwa ni sehemu ya mafunzo waliyoyapata, Pia jumla ya watoto ambao hufika kila siku kwa ajili ya mafunzo ni kuanzia jumatatu mpaka Ijumaa ni watoto 15.
Hivyo wewe ukiwa kama mwaajili wa mtoto wa ndani mpatie ridhaa mtoto huyo ili ajipatie uzoefu ambao utamsaidia baadaye katika maisha yake, Hatubomoi ila tunawajengea pia uwezo wa kushi vema na waajili wao na kutambua haki zao za msingi wanapokuwa kwa waajili wao, Kushiriki ni bure wala hakuna kiingilio chochote cha pesa au njia yoyote ya malipo kwa mfanyakazi wa ndani, zaidi ni kuzingatia masharti na kuja kwa wakati aliochagua mwenye, Zaidi ni  kujaza fomu ambayo itamtambulisha yeye kama mmoja wa washiriki wa watoto wafanyakazi wa ndani katika Shirika hilo, Wanapatikana  Isamilo Jijini Mwanza  “Tuwape sauti watoto wafanyakazi wa ndani”
Karibuni sana kwa mawasiliano zaidi S.L.P 11348 Namba ya simu  +255 717-118087 na +255713-137222 Mwanza-Tanzania.
 Hawa ni baadhi ya wanafunzi ambao wanapata mafunzo mpaka sasa ya cherehani.
Mwanafunzi katika mafunzo ya kompyuta akiwa anajifunza mwenyewe baada ya kupata uzoefu toka kwa mwalimu wa mafunzo.
 Mwanafunzi akiwa anashona kwa umakini sana na akitabasamu juu ya ujuzi alionao sasa.
 Huyu ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo linaloitwa Chezesha Mikono akitoa maelekezo kwa mwanafunzi juu ya ushonaji wa nguo.
 Mwanafunzi akitengeneza kikapu kwa umahili sana na anafuraha sana
 Kijana huyu anajituma sana tena kwa bidii katika mafunzo yake ya kila siku katika shirika hilo.
Mwalimu wa wanafunzi hao akionyesha uwezo alionao katika kushona nguo
Picha na Habari: Ramso Kassim Jijini Mwanza.

1 COMMENTS:

Anonymous said...

Pongezi kwa kazi nzuri ya kukusanya taarifa.

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster