June 17, 2011

Tuzo kutoka Ubalozi wa Marekani

Hi | 3:08:00 PM |
Kivulini ni Shirika lisilo la Kiserikali linalotetea haki za wanawake na watoto wanaonyanyasika majumbani lililoanzishwa tangu mwaka 1999, Nia na malengo ya Shirika hili ni kuona familia zikiwa salama na zenye amani, Mkurugenzi wa shirika hilo lisilo la Kiserikali Kivulini Bi. Maimuna Ahmad Kanyama alifanikiwa kwa mwaka huu kunyakua Tuzo ya Mwanamke Shujaa, Jasili na Shupavu Tanzania kwa kutetea haki za wanawake na watoto wanaonyanyasika majumbani, Tuzo hiyo ilitolewa na  Ubalozi wa Marekani  tarehe 8/03/2011,Vikundi mbali mbali kutoka Kata ya Mahina pia wameandaa maandamano ya kumpongeza kwa ushindi huo na kiongozi mwandaaji wa maandalizi ya Maandamano hayo ni Mh, Steven Magembe Nyashilu ambaye hufahamika kwa jina la Magembe na alisema Katika sherehe hiyo ya kumpongeza Bi. Maimuna Ahmad Kanyamala kutakuwa na burudani aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na Ngoma za asili, Maigizo, kumvisha Taji la ushindi na mengineyo pia kwa washiriki wote watakuwa na fursa ya kumpatia zawadi waziloandaa kwa ajili yake, itakuwa siku ya tarehe 18/06/2011 kuanzia saa 7 Mchana mpaka saa 11 Jioni katika Kata ya Mahina ofisi ya Mtendaji wa Kata Mwanza, Hivyo basi wewe ukiwa kama mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto unakaribishwa sana.
 Bi. Maimuna Ahmad Kanyamala wakati wa Maandamano ya kumpokea kutoka  Dar es Salaam Mara tu baada ya kupokea Tuzo toka kwa Ubalozi wa Marekani
 Akipewa Ngao kwa ishara ya Ushujaa na Ujasili
Pichani ni Tuzo ya Bi. Maimuna Ahmad Kanyamala Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wanawake na Watoto Jijini Mwanza.
 Huyu Ndiye Mh, Steven Magembe Nyashilu ambaye hufahamika kwa jina la Magembe muhamasishaji wa kujitolea kutoka Kata ya Mahina.


2 COMMENTS:

Anonymous said...

Dear Ramso

I have visited your blog you are doing a great job congratulation.
God Bless You
Mama Nyenga

Anonymous said...

Asante sana Mama Nyenga Karibu tena kwa mara nyingine

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster