Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akisistiza jambo kwa watangazaji wa
vipindi vya redio mbalimbali (hawapo pichani) kuhusu vigezo na masharti
vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni
bingwa" itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kushinda tiketi 2 kila
wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United
na mamilioni ya pesa kila siku.Kulia kwake ni ofisa wa matangazo wa
Airtel Bw. Abdallah Gunda.
kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airte Tanzania Bw Jackson Mmbando
akibadilishana mawazo na watangazaji wa kipindi cha jahazi bw Musa
Huseni (kati) na Ephraem Kibonde mara baada ya mkutano maalum na
watayarishaji na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio kwa lengo la
kuwaeleza vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni
mpya ya Airtel Mimi ni bingwa" inayowawezesha wateja wa Airtel kushinda
tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya
Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.
0 COMMENTS:
Post a Comment