
BALOZI wa Pepsi, Juma Kaseja ni miongoni mwa wa wadau wa soka walioalikwa kushuhudia fainali ya kuwania kombe la Meya wa Jiji la Mwanza (Meyor’s Pepsi Cup ), Stanslaus Mabula.
Mlinda mlango huyo namba moja wa timu ya taifa (Taifa Stars) ataungana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala Katibu Mkuu wa TFF na Angetile Osiah.
Wengine ni Memeya wa Majiji na Miji ya Dar es Salaam Jerry Slaa,
Gaudensi Lyimo wa Arusha, Kapinga wa Mbeya, Omari Nondo wa Morogoro,
Moshi na Bukoba.
Fainali hiyo itafanyika Agosti 10 mwaka huu ambapo bingwa
atajinyakulia pikipiki ya magurudumu matatu (Bajaj) na shilingi milioni
moja, kombe kubwa na dogo na medali za dhahabu wa pili ataibuka na
kitita cha shilingi 1.5 milioni, kombe na medali ya fedha.
Mshindi wa nafasi ya tatu akipata kifuta jasho cha shilingi 500,000
ambapo timu yenye nidhamu itapata kombe na mfungaji bora atatwaa kiatu
cha dhahabu (Golden boot).
Kufikia hatua hiyo Kata ya Mkolani anakotoka Meya Stanslaus Mabula,
iliigagadua Polisi Jamii kwa penati 5-4 baada ya kutoka suluhu, huku
Isamilo ikiiondosha Mbugani kwa bao 1-0 katika nusu fainali ya pili.
Timu mbili za Polisi Jamii na Mbugani zilizokuwa kundi C la uwanja wa
Polisi Mabatini lililotajwa kuwa la kifo, zitakutana kusaka nafasi ya
mshindi wa tatu wa michuano hiyo.
Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo, Paul Maganga, fainali
itachezwa kwenye uwanja wa Nyamagana Agosti 10 mwaka huu, itatanguliwa
na mechi ya kusaka mshindi wa tatu hapo Agosti 9, mwaka huu kwenye
uwanja huo huo.
Washindi watachuana kwenye fainali huku washindwa wakicheza kuwania nafasi ya tatu.
Bingwa wa michuano hiyo atawajibika kukaa na kombe kubwa kwa wiki
moja kabla ya kulikabidhi katika ofisi za Meya ambapo jina bingwa
litaandikwa kwenye kombe hilo kwa kutambua ushindi wake.
Michuano hiyo imedhaminiwa kwa miaka mitatu na kampuni ya SBC Pepsi
inayotengeneza na kuzalisha vinywaji baridi, ambapo wadhamini wenza ni
kampuni ya simu ya Vodacom, Dume Kondomu na Barmeda Televisheni.
0 COMMENTS:
Post a Comment