Habari iliyotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa filamu nchini
Jaji Khamis (Kashi)aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa
na wasanii kama mzee masinde,samson na wengine katika mchezo wa Tamu
chungu na mingine mingi Amefariki dunia mchana huu katika hosptali ya
taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.
Taarifa za awali zinasema kuwa alikuwa amelazwa hapo kwa muda
kiasi kabla ya kufikwa na mauti hayo. Tutaendelea kuwajulisha zaidi
punde tutakapoendelea kupata taarifa zaidi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Ameni
0 COMMENTS:
Post a Comment