Mumewe amgonga na gari na baada ya Nasra
mkewe kuanguka akanasa chini ya gari ya mumewe na kumburuza umbali wa mita 150

Marehemu Nasra aliumia sana ngozi yote ya mgongoni,mbavuni,makalio,ikavuka na kubaki kwenye lami.Sikio lake la
kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7 zilivunjika pamoja na mguu.
Nasra pichani kulia mwenye kilemba chekundu akiwa na ndugu zake wakati akiwa mzima.


Nasra pichani kulia mwenye kilemba chekundu akiwa na ndugu zake wakati akiwa mzima.
Picha ya muwewe Elia Makumbati ambae
mpaka sasa anatafutwa na jeshi la polisi kwa kitendo cha kinyama
alichokifanya.Jeshi la polisi mkoani Mara wanafanya juhudi za kila namna
kumkamata lakini amekuwa akikimbia mara aonekane Kenya,Botswana na
kwengineko lakini bado hajakamatwa.Kwa utakae muona usisite kutoa ripoti
zake.Mpaka askari wa upelelezi wa kimataifa interpol ina taarifa zake.
Wiki iliyopita tuliongea katika leo
tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra pichani.Mama huyu alikuwa mkazi wa
Bunda mkoani Mara lakini Dar es salaam alifika kufanya matibabu katika
hospital ya Muimbili.Kwa miaka takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia
Makumbati na kujaaliwa kupata watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu
cha UDOM.Kwa miaka yote wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama
akiwa anapigwa sana hata kuchanwa na viwembe.
Mwezi wa pili walitofautiana baada ya
bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa wametofautiana na Nasra kuendelea na
maisha siku hiyo bwana akamfata akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa
na rafiki yake wanatembea akamfungia breki mguuni akamwambia anataka
kuongea nae.Nasra akakataa akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea
nae kama vipi amfate nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule
akamfata kwa nyuma akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa
chini hivyo kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika
kwenye tuta akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.
Kiukweli aliumia sana sana ngozi yote
ya mgongoni,mbavuni,makalio,ikavuka na kubaki kwenye lami.Sikio lake la
kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7 zilivunjika pamoja na
mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa Bugando Mwanza lakini ikawa
anahitajika kuhamishiwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa
muhimbili alikuwa na hali mbaya sana baadae ikathibitika kuwa ameumia
ndani kwa ndani kwani alibadilika sana akavimba na kuwa mweusi.Kwamuda
wote wa miezi takribani sita alikuwa katika maumivu makali na bahati
mbaya hakuweza kupambana tena kupigania maisha yake.
Usiku wa kuamkia jumanne ya tarehe 10
Nasra akaaga dunia.Ilikuwa ni huzuni sana jinsi alivyoteseka na namna
mazingira ya kifo chake kilivyotokea.Tulikuwa na matumaini kuwa angeweza
kupona maana dakika za mwisho alikuwa anaongea japo kwa shida.
Tunaomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Nasra mahala pema peponi,Amina.
0 COMMENTS:
Post a Comment