December 7, 2012

MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUSHIRIKI MAPENZI NA MWANAE WA KUMZAA

Hi | 5:06:00 PM |
Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya BwanaYussuf Hamad (39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi  wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
 Hapa bwana Yussuf Hamad akitoka mahakamani kwa aibu
Hapa jamaa akijitahidi kukwepa kamera za waandishi wa habari 
Binti huyo ambaye alipewa mimba na baba yake mzazi amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu, binti huyo kaletwa jana mahakamani hapo kama ushahidi wa kesi hiyo na kesi imehairishwa mpaka tarehe 12/12 mwaka huu.
 
Hapa akiwatishia na jiwe watu waliokuwa wakimuzomea baada ya kutoka mahakamani

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster