Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya Barclays
Tanzania, Tunu Towo Kavishe (kushoto) akionyesha jezi halisi ya timu ya
Arsenal ikiwa ni moja ya zawadi watakazopewa washindi wa promosheni ya
Ligi Kuu ya England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo. Mshindi mmoja
katika kila droo hujishindia tiketi ya yeye na mwenzake kwenda
kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo nchini Uingereza. Droo hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Maggid Bakari na Mkuu wa Bidhaa,
Huduma na Utafiti wa benki hiyo, Samwel Mkuyu.
Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Rukia
Kizwi (kushoto) akitoa tiketi ili kumpata mmoja wa washindi wa
promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo.
Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia tiketi ya yeye na mwenzake
kwenda kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo nchini Uingereza na wengine
wawili hujishindia zawadi ndogondogo. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar
es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa
Barclays, Tunu Towo Kavishe, Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa benki
hiyo, Samwel Mkuyu, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari
Maggid na Ofisa Mawasiliano wa Barlclays, Lilian Machare.
0 COMMENTS:
Post a Comment