Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) nchini Tanzania Bw. Emmanuel
Kalenzi akifafanua shughuli za Shirika hilo na mafanikio yake hapa
nchini ambapo mpaka sasa limeshachagua maeneo yatakayofadhiliwa chini ya
‘Global Environment Facility- GRF’ kwa miradi kadhaa katika mikoa ya
Morogoro, Njombe na Rukwa.
Akizungumza wakati wa wiki ya
maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa amesema katika kutimiza
malengo ya UNIDO ambayo ni kukuza uzalishaji viwandani na kupunguza
umasikini, shirika hilo linafanya kazi bega kwa bega na serikali na
jamii kwa ujumla katika kuongeza ushiriki wa wananchi katika vikundi ili
kurahisisha maendeleo.
0 COMMENTS:
Post a Comment