October 19, 2012

VURUGU ZANZIBAR, MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA

Hi | 10:17:00 PM |
Vurugu zimeibuka Zanzibar, inasemekana kufuatia kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la Uamsho linaloendesha mihadhara ya dini ya Kiislam na kampeni za kuvunja Muungano, Sheikh Farid. Askari wa kutuliza ghasia wanapiga mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa kundi hilo ambao wanachoma matairi na kurusha mawe kwa askari.

Inasemekana vurugu hizo zimefikia kiwango cha kusababisha barabara za eneo la Darajani mjini Unguja, kufungwa. Wafuasi hao wa Uamsho wanaandamana kushinikiza polisi wamwachie huru kiongozi wao huyo. Chini ni baadhi ya picha ya kilichotokea mchana huu huko.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster