August 29, 2011

VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAPITISHA MAAZIMIO MANANE

Hi | 7:30:00 PM |
Mkutano wa Wakuu wa vyama vya ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika umemalizika  Mjini Windhoek Namibia hapo  jana na kupitisha  maazimio manane tayari kwa utekelezaji.
Maazimio hayo ni pamoja na kuvitaka   vyama vya ukombozi kushirikiana na Umoja wa Afrika –AU na Shirika la umoja wa Mataifa la Elimu sayansi na Utamaduni – UNESCO kuhifadhi maeneo ya kihistoria ambayo yalitumika wakati wa kutafuta uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika.
Akitoa ufafanuzi wa namna maeneo hayo yatakavyo hifadhiwa Mwenyekiti wa CCM , Rais Dkt. Jakaya Kikwete amesema kila chama kilichoshiriki katika vita vya ukombozi kusini mwa Afrika kitakagua eneo lake hapa nchini kisha kulitambua na kushirikiana na Tanzania katika kuhifadhi eneo lake.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Wilson Mukama amesema upo umuhimu  wa makada wa vyama hivyo kualikana katika maadhimisho mbalimbali
Mkutano huo ulihudhuriwa  na rais  Dkt. Jakaya Kikwete wa Tanzania, Hifikepunyepohamba wa Namibia, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Makamu wa Rais wa Angola Roberto De Almeida, Katibu mkuu wa chama cha ANC Gwede Mantashe na Filipe Paunde katibu mkuu wa chama cha FRELIMO.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster