Migambo wakilanda mitaani na barabarani kusaka watupa taka ovvyo katika kila sehemu kama unavyoona pichani
Usiombe kukutwa na hawa binadamu walinzi wa Jiji la Mwanza ni Hatari sana
Wako makini sana kutazama raia na unapopita wanakuanzia kichwani mpaka mguuni.
Ili kuboesha mazingira kuwa safi na salama katika Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Jiji la Mwanza imetunga sheria mpya ndogo ambayo itahusisha utunzaji wa takataka mahali panatohusika kuliko kutupa kila sehemu ya mji ambapo huchafua mji, Ukijumuisha kila aina ya taka mfano, Ganda la Vocha, Miwa, Pipi, Mifuko ya maji pamoja na chupa na vinginenvyo, Hivyo Halmashauri imekaa na kuandaa wanamigambo ambao watakuwa kutwa nzima wakiznguka kila sehemu kwa ajili ya kuhakikisha kila kona au pande ya mjini ni safi. Unapokutwa na wanamgambo hawa hukuchukua na kukulazimu kutoa faini ya pesa Taslimu ya Kitanzania elfu 50,000/= Hivyo ni vema unapopata taarifa hii mwalififu na mwenzako.
0 COMMENTS:
Post a Comment