Hili ndilo eneo la Mabatini Jijini Mwanza ambapo kuna wingi au mlundikano wa watu takribani wasiopunguza laki 2 na kuendelea ambao huweka jam hasa wakati wa Asubuhi tukiwa tunawahi ofisini na Jioni wakati wa kutoka kubangaiza kwa ajili ya familia na mengineyo, Ki ukweli eneo hili ni kero kubwa kwa sisi ambao tunapitia njia hiyo ya mabasi ya Mikoani kwani ukiwa na lengo la kuwahi asubuhi katika kazi na shughuli zako binafsi weka na muda wa ziada kuuacha eneo hilo kwani Jam yenye huanzia sehemu moja inayoitwa Buzuruga mpaka Mabatini ambapo unaweza kuwa na msururu wa zaidi ya magari 40 na kuendelea..!! Serikali angalia hilo japo wajengewe hata njia ya kuvuka kwa kupitia juu au la kwani pia ajari sehemu hii huwa ni mara kwa mara hutokea, hali hii inatishia hata amani ya wakazi wanaoishi eneo hilo husubiri zaidi ya dk 20 mpaka 30 kwa ajili ya kuvuka barabara.
Mwenye macho aambiwi ona wala Tazama utaona mwenyewe kwa mimacho yako, na nilibahatika kupiga picha ambayo ilikuwa watu si wengi sana ila kwa wakati mwingine nitaleta picha halisi zaidi ya hii
Wakati mwingine hata hawa maafisa usalama hupata wakati mgumu sana kuongoza watu na magari kwa kweli huchoka sana kwani wakati wote mikono huwa mbele na nyuma kama unavyoona pichani
Hapa ni kwa Ancle wangu anayeitwa Ntobi pia ni mwenyekiti wa maeneo ya Mabatini, Huuza Cd, DVD, VHS, Hutoa Photocopy na mengineyo ikiwa ni pamoja na M-Pesa, Tigo -Pesa, Na StarTimes Credit, Pia hupatikana kwa Namba ya Simu +255 755- 738181 karibuni sana kwa Huduma Bora na ya Haraka zaidi kwa Mteja, Karibuni pia katika Makazi ya Mji wa watu wengi Mabatini Jijini Mwanza.
1 COMMENTS:
inatisha sana kwa kweli wala hata si uongo
Post a Comment