
Watafiti toka
kampuni ya utafiti ya Zscalar wamegundua kuwa,tovuti za kichina
zenye picha za ngono zimekuwa zikisambaza virusi ambavyo vinasababisha simu za
mikononi kushambuliwa na virusi vya komputa viitwavyo malware.
Utakapotembelea tovuti hizo na ukajaribu kuangalia video,tovuti itakuomba upakue sehemu ya program ya komputa ambayo kiuhalisia ni kirusi kiingine kiitwacho trojan.
Kirusi hicho cha Trojan kinajishajilisha chenyewe kwenye simu yako na kuifanya simu yako kuwa na uwezo wa kupokea matangazo yanayohusisha ujumbe mfupi wa maneno (sms) ulioko kwenye simu yako.Jambo ambalo litasaidia wahalifu wa mtandao kudukua taarifa zako za kibenki kwenye simu iliyo na kirusi hicho kiurahisi.
0 COMMENTS:
Post a Comment