February 18, 2015

MTUMIAJI WA FACEBOOK AKIFARIKI NINI KINAFANYIKA!

Hi | 7:27:00 PM | |
Mitandao ya kijamii imetusogeza karibu, Facebook ni moja ya mitandao hiyo, lakini kurasa za mtumiaji wa mtandao kama Facebook huwa zinaendelea kuwepo hata kama ikitokea mtumiaji amefariki.

Facebook wameenda mbali zaidi, muda si mrefu kutakuwa na setting ambayo mtumiaji wa mtandao huo anaweza kuamua kama ukurasa wake huo ufutike au uendelee kuwepo huku ukiendeshwa na mtu mwingine, au ubaki kwa ajili ya kumbukumbu za mtumiaji kama ikitokea mtumiaji amefariki.

Hii itaanza kufanya kazi hivi karibuni Marekani na baadaye wataalam wa Facebook wanaangalia namna ya kila mtumiaji kuweza kuufanya hivyo ukurasa wake wa Facebook.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster