February 18, 2015

KAMPUNI 3 KUBWA ZIMESITISHA KURUSHA MATANGAZO YA TV KWA MUDA WA SIKU 3

Hi | 7:32:00 PM | |
Kampuni tatu kubwa za utangazaji zimesitisha kurusha  matangazo kwenye televisheni kwa muda wa siku tatu baada ya Serikali kudhibiti mitambo ya zamani ya kurusha matangazo kwa mfumo wa analojia huku Kampuni hizo zikiwahakikishia waandishi wa habari kuwa hawatawafukuza kazi. 
Kampuni hizo za Standard Media, inayomiliki television kibinafsi ya KTN na National Media Group inayomiliki NTV na QTV pamoja na Royal Media Services inayomiliki Citizen TV zimekuwa katika malumbano na Serikali ya Kenya kuhusu uhamiaji wa kurusha matangazo kwa kutumia mfumo wa digitali kutoka analojia.


Hata hivyo wasimamizi wa vituo hivyo wametumia njia ya mitandao kurusha matangazo yao, huku halmashauri ya Mawasiliano nchini humo  imewataka waende mahakamani ili kufikia muafaka juu ya wala hilo.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster