Katika baadhi ya sehemu duniani watu
wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao
mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini
ya kiwango,
hii hupelekea watu
hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine
kubadilisha ngozi zao.
Tafiti zinaonyesha
kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi
ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa
kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha
kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa
kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati
ya krimu au vidonge.
Mtu anaeyejichubua
anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa
nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata
watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika
kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha
zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa
mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine
hujitokeza kadri mtu anavyotumia
0 COMMENTS:
Post a Comment