Jengo la TTCL, Makao makuu,
EXTELECOMS limeungua moto kuanzia majira ya leo saa 12:00 asubuhi hadi saa
1:20.
Moto huo ulikuwa unawaka katika
ghorofa ya sita ya jengo hilo na ulikuwa unawaka katika vyumba vitatu kwa mara
moja.
Mwandishi wetu alifanikiwa
kufika katika jengo hilo na
kujionea mishe mishe za wafanyakazi
wakiondoa magari yao na magari ya shirika hilo kongwe nchini.
Magari ya kikosi cha zimamamoto
kutoka kikosi cha ukoaji cha Jiji la Dar es Salaam yaliwasili saa 12:20, lakini
kulikuwa na ubishani kati ya wafanyakazi wa zima moto na wale wa TTCL, baada ya
wafanyakazi wa Zimamoto kulaumu kuwa walienda pale siku kadhaa zilizopita
kukagua jengo lakini walifukuzwa kama mbwa,
Licha ya Kikosi hicho kuwahi
hawakuwa na maji yenye pressure na ngazi za nje kufika hadi ghorofani, hali
iliyopelekea watu kutumia ngazi za ndani kuingia kwenye jengo hilo hali ambayo
ni hatari kwa maisha yao.
Gari ya Ultimate Security
walifika mnamo saa 12:30 na kwa ushirikiano moto uliweza kufanikiwa kuzimwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment