September 18, 2013

FRANCIS CHEKA NAHITAJI KUWA MPYA KIELIMU ILI NIFIKE MBALI NAAMUA KUANZA KIDATO CHA KWANZA

Hi | 1:18:00 AM | | |
Bingwa wa dunia wa WBF Francis Cheka ambaye hivi karibuni alipewa zawadi ya  kiwanja na Rais Jakaya Kikwete baada ya ushindi wake dhidi ya bondia wa Marekani, ameamua kurudi shule.Cheka anasema hakupata nafasi ya kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba. “Mimi sikusoma niliishia darasa la saba, lakini nimeamua kurejea darasani baada ya kupewa udhamini na shule ya St Joseph”.

“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine “.Habari kamili ipo kwenye gazeti la Mwananchi la Sept 17.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster