Mtandao wa ‘google’ unaotumika kutafuta mambo tofauti tofaauti mtandaoni kwa njia ya ‘key’ word imekua msaada mkubwa kwa wanaotumia kwa matumizi mazuri.Mtandao huu unaweka kumbukumbu za neno au ‘key word’ linalotafutwa mara nyingi zaidi na kua katika nafasi za juu za majibu inayotoa baada ya mtumiaji kuingiza neno hilo.Mwandishi wetu katika harakati za kutaka kujua ‘watanzania’ tunatambulika vipi katika ulimwengu wa mtandaoni ndipo alipokutana na majibu ya aibu.
Neno lililoongoza ni ‘KUKAMATWA‘ huku likifuatiwa na maneno mengine ya aibu ambayo watu wengi wamekua wakiyatafuta kupitia mtandao huo mengine yakiwa ni matusi.Unaweza kujaribu kuingiza neno lingine mfano ‘WAKENYA’ ili uone majibu utakayojibiwa pia.Tunapenda kushauri watumiaji wote wa mtandao kutumia mtandao katika shughuli za maendeleo binafsi na jamii kwa ujumla,pia kuelimisha na kujiendeleza katika nyanja tofauti tofauti.
0 COMMENTS:
Post a Comment