Makardinali wamemchagua Baba Mtakatifu mpya kuliongoza Kanisa Katoliki katika karne hii ya 21. Vilio vya furaha vilitawala wakati moshi mweupe ulipoonekana kwenye anga la Vatican City muda mchache uliopita. Shughuli hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na waamin wa dhehebu hilo kubwa duniani hatimaye imekamilika, na papa mpya atakayeliongoza kanisa ni Cardinali Jorge Bergoglio Raia wa Argentina. Na jina la upapa atakalokuwa anatumia ni Francesco The first Mwenye umri wa miaka 70 baada ya kuchaguliwa papa alitoka na kusimama dirishani kama kawaida na kuwabariki watu waliokusanyika nje katika uwanja wa kanisa la St. peter kwa kuwapungia mkono.
0 COMMENTS:
Post a Comment