February 19, 2013

TASWIRA ZA SHEIKH PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI CHINI YA ULINZI MKALI

Hi | 12:02:00 AM | |
 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda (katikati) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati kesi inayomkali ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Katibu huyo na wenzake 49 ilipoanza kusikilizwa
Watuhumiwa  54 wanaokabiliwa na shtaka la kuandamana isivyo halali kushinikiza kuachiwa kwa dhamana kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi  atika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati kesi inayomkabili Shikh Ponda Issa Ponda ilipofikishwa
Mfuasi wa Sheikh Ponda Issa Ponda akijitetea mbele ya Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) baada ya kutolewa amri ya kuondoka  katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati kesi inayomkabili Sheikh huyo ilipoanza kusikilizwa
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda akirudishwa rumande.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster