February 12, 2013

TASWIRA ZA MV VICTORIA YANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO JIJINI MWANZA

Hi | 7:54:00 PM | |
Wafanyakazi wa Melini wakishirikiana na kikosi cha zima moto wakifanya jitihada za kuzima moto huo.
Ndani ya masaa mawili moto huo ulikuwa umedhibitiwa na kikosi cha zima moto na uokoaji waliowasili katika eneo
Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini(MSC)imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea sehemu mojawapo ya Meli hiyo.
Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zlizo patikana toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto ulipoangukia katika sehemu ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.


wa upande wake afisa mfawidhi wa Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa majini na nchi kavu(SUMATRA) kanda ya ziwa Josephat Loisimaye amesema kuwa uzembe wa viongozi wa MSC ndio ambao ulisababisha kutokea kwa moto huo.
Amesema kuwa viongozi wa MSC walipashwa kuchukua tahadhari mapema kabla ya kuanza uchomeleaji katika sehemu ya Meli hiyo na kueleza kuwa wanasubiri ripori ili waweze kuchukua hatua zaidi.
Hata hivyo Loismaye amesema kuwa Meli ya Mv Victoia iko salama na itaendelea na safari zake kwenda Bukoba leo usiku kwa kuwa moto huo haukuweza kuathiri mfumo wa injini ya Meli na kukipongeza kikosi cha zimamoto kutokana na kufika mapema na kuzima moto huo vinginevyo Meli hiyo ingeliteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster