Hii ni taswira ya basi la Sabena lenye nambari za usajili T800 AZU jinsi lilivyopata ajari mbaya na kupelekea vifo vya watu wasiopungua 6 maeneo ya Tinde kilometa chache kufika mzani.
Mzungu ambaye ni mtalii pia aliyekuwa akiendesha Farasi pichani alinusurika kifo na kuvunjika mguu wake akiwa anasikilizia maumivu makali.

Pichani ni mwili wa mtalii wa kizungu wa kike aliyepoteza maisha papo hapo baada ya ajali kali sana iliyosababishwa na farasi wawili waliokuwa wakiwaendesha wazungu hao wawili.
Chini ni mwili wa mtalii wa kike aliyepoteza maisha katika ajari hiyo, Pembeni yake ni mume wake akiamwangalia kwa uchungu marehemu mke wake.
Gari lenye usajiri wa namba T800 AZU Sabena lapata ajari mbaya maeneo ya Tinde na kuua watu zaidi ya 5 papo hapo,
Chanzo cha ajari hii kilisababishwa na watalii wawili wa kizungu wa nchi za ughaibuni ikiwa jinsia ni mke na mme ambao walikuwa na Farai wawili wakiwaendesha kuelekea Mkoani Tabora, Inasemekana Farasi hao walikuwa mwendo kasi sana kiasi kwamba walikataa kutoka barabarani na kupelekea ajari ya magari matatu ikiwa ni Sabena, Master City na Lori kubwa lililokuwa limebeba siment. Baada ya ajari hiyo mzungu mmojawapo jinsia ya kike alipoteza maisha papo hapo na mwingine kuvunjika mguu.
0 COMMENTS:
Post a Comment