Kibaka anayesadikika kuiba betri ya gari aina ya Fusso karibu na viwanja vya furahisha Hotel ya Annox Jijini Mwanza alipigwa kwa kutumia tofali kwenye miguu yake na kuvunjwavunjwa kabisa kabla ya kifo chake pichani akilalamika dhidi ya maumivu makali sana
Taswira za maumivu makali ya kibaka kabla ya kifo chake baada ya kupigwa kipigo kikali na wananchi wenye hasira kali.
Ikiwa ni majira ya saa tisa usiku eneo la Viwanja vya furahisha Jijini Mwanza Hotel ya Annox kijana mmoja mwenye umri unaokadiliwa kuwa miaka 26 akamatwa akiiba Betri ya gari aina ya Fusso na kupigwa vibaya na wananchi wenye hasira kali na kupelekea kifo chake tukio ambalo lilichukua muda wa masaa matatu,
Chanzo cha habari kinasema kuwa kuna mlinzi wa nyumba ya pili aliyekuwa katika eneo la lindo aliweza kupepesua jicho lake na kuwaona vibaka watatu wakitoka kwa kasi huku wakiwa wamekamatilia betri kubwa yenye nguvu ya N120, Baada ya kuona tukio hilo aliamua kutoa taarifa kwenye Hotel hiyo ya Annox eneo la viwanja vya furahisha Jijini Mwanza sehemu ambayo tukio lilitokea, Waswahili wanasema siku za mwizi ni arobaini na sikio la kufa halisikii dawa, Vijana hawa walirudi kwa mara nyingine na waliwekewa mtego wa kuwanasa na walifanikisha kumshika kibaka mmoja aliyepigwa na wananchi wenye hasira kali kipigo cha mbwa na hii inatokana na tamaa ya fedha na hali ngumu ya kujikimu kimaisha kwani wimbi la vijana wengi wamejiingiza katika masuala ya wizi.
0 COMMENTS:
Post a Comment