Mtoto mwenye umri wa miezi saba, Anjela David, anadaiwa kuuawa na mfanyakazi wa ndani
Mtoto
mwenye umri wa miezi saba, Anjela David, anadaiwa kuuawa na mfanyakazi
wa ndani jijini Dar es Salaam na kisha kutoroka na mizigo yake. Baba mzazi wa mtoto huyo, David
Salakana, mkazi wa Sinza Afrika Sana alisema kuwa tukio hilo lilitokea
juzi, ingawa hana uhakika na muda kamili kitendo hicho kilipofanyika. Alisema
kuwa juzi majira ya asubuhi aliondoka na mkewe kwenda katika shughuli
zao na kumuacha mtoto wao akiwa na mfanyakazi huyo aliyemtaja kwa jina
moja la Marietha (19).
Salakana
alisema mkewe, Anna Haule, ilipofika majira ya mchana alimpigia simu
mfanyakazi huyo ili kufahamu hali ya mtoto wao kama tayari ameshampatia
chakula au la. Alieleza
kuwa mfanyakazi huyo baada ya kupigiwa simu hiyo alijibu kuwa haelewi
kama mtoto huyo amekula au la na kwamba yeye (Marietha) hayupo ameondoka
zake.
Alisema baada ya kumjibu hivyo, mkewe aliamua kumpigia simu kijana mmoja ambaye alimtaja kwa jina moja la Ally ambaye ni jirani yake na kumuomba aende nyumbani kwake na aingie ndani na kumuangalia mtoto huyo. Salakana alisema kijana huyo baada ya kufika alimkuta mtoto huyo akiwa amelala na alipojaribu kumuamsha hakuamka ndipo alipomueleza mkewe kuhusiana na hali hiyo. Hata hivyo,
Alisema baada ya kumjibu hivyo, mkewe aliamua kumpigia simu kijana mmoja ambaye alimtaja kwa jina moja la Ally ambaye ni jirani yake na kumuomba aende nyumbani kwake na aingie ndani na kumuangalia mtoto huyo. Salakana alisema kijana huyo baada ya kufika alimkuta mtoto huyo akiwa amelala na alipojaribu kumuamsha hakuamka ndipo alipomueleza mkewe kuhusiana na hali hiyo. Hata hivyo,
Salakana alisema baada ya mkewe kupatiwa taarifa hizo alirudi
nyumbani ghafla na ndipo alipoamua kumchukua mtoto wao na kumpeleka
katika Hospitali ya Marie Stopes iliyoko Sinza ili kumuangalia kama ni
mzima au la na ndipo alipojulishwa kuwa alishafariki dunia. “Kutokana
na mazingira hayo, nashindwa kukueleza kuwa mwanangu amefariki muda
gani kwani muda ya mchana ndipo niliporudi na kumchukua na kumpeleka
hospitali, sijaelewa vizuri kifo cha mwanangu kwani tulimuacha akiwa ni
mzima halafu namkuta ni marehemu cha ajabu mfanyakazi katoroka na mizigo
yake,” alisema Salakana. Salakana
alisema wakati anaingia chumbani alikuta chakula aina ya mtori kipo
chini. "Sasa sijaelewa kama alimlisha mtoto chakula au la,” alisema. Alisema
tayari amekwisha kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha Kijitonyama,
lakini mfanyakazi huyo ambaye anatokea Mkoa wa Shinyanga hajapatikana. Alisema
mfanyakazi huyo baada ya tukio hilo, alifunga mizigo yake yote na
kuamua kuondoka nyumbani hapo na kuelekea kusikojulikana huku simu yake
ya kiganjani ikiendelea kuita bila kupokelewa.
Salakana alisema mfanyakazi huyo amekaa naye kwa muda mrefu na kwamba alimpata kupitia kwa dalali. Alisema
wamekuwa wakiishi na msichana huyo kama ndugu yao na kwamba hawajawahi
kumgombeza kwa chochote,
ingawa walimsisitiza suala la usafi kwa mtoto
huyo na kuhakikisha anampatia chakula kwa wakati. Aidha,
Salakana alisema kuwa majibu waliyopatiwa kutoka kwa daktari
yameonyesha kuwa mtoto huyo katika sehemu za mgongo wake amepigwa na pua
zake zimeminywa. Alisema
jana jioni walitarajia kufanya kikao cha ndugu na baada ya hapo watatoa
maamuzi kuhusiana na tukio hilo na kwamba mwili wa mtoto huyo
unatarajia kusafirishwa leo kwenda Rombo mkoani Kilimanjaro. Akizungumza
kwa masikitiko, Salakana alisema kuwa kuna jirani yake ambaye alikuwa
akimtafuta ili amweleze kuhusiana na mfanyakazi huyo alivyokuwa
akimfanyia vitendo vibaya mwanaye. Alisema
jirani yake alimueleza kuwa wakati Marietha akiwa anamlisha mtoto huyo
chakula, alikuwa anamtukana matusi makubwa ambayo hayaendani na umri wa
mtoto na wakati mwingine alikuwa anampiga. “Huyu
mfanyakazi sijui ni kwanini sikumuamini sana kwani hata nikiwa kazini
nilikuwa narudi mapema na kuamua kushinda na mwanangu hapa dukani,”
alisema.
Mwanangu amefariki katika mazingira magumu, sielewi amemuua kwa
kitu gani na kama sio yeye ni kwa nini aliamua kukimbia na mizigo yake
yote?” Alihoji Salakana. Mama wa mtoto huyo, alishindwa kuzungumzia tukio hilo kutokana na uchungu aliokuwa nao. Naye
bibi wa mtoto huyo, Beatrice Ndemasi, alisema kuwa kifo cha mtoto huyo
kimewasikitisha kwa kuwa kimetokea ghafla kwani hakuwa mgonjwa. Ndemasi
alisema mjukuu wake alionekana kwenye mgongo wake kuwepo na alama
ambazo zilivimbia damu alipofikishwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH).
Alisema mwili wa mjukuu wake kwa sasa umehifadhiwa MNH kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi leo asubuhi. Alisema
wanategemea uchunguzi huo utawapatia majibu ili wabaini
kilichomuua.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Kamanda Kenyela amesema wanaendelea kumtafuta mfanyanyakazi huyo wa ndani kwa tuhuma za mauaji. Alisema
mfanyakazi huyo aliachiwa mtoto na wazazi walipokwenda katika shughuli
zao za kila siku na kumkuta ameshafariki naye akaondoka. Kamanda Kenyela alisema ni lazima msichana huyo akamatwe kuhusiana tuhuma za tukio hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment